Pambazuko FM Radio
Pambazuko FM Radio
13 June 2026, 13:52

“Elimu ya ufundi stadi ni ujuzi muhimu unaotolewa chuoni, na ujuzi huo unamwezesha kijana kujitegemea na kuepuka utegemezi.”Mwalimu Peter Magoda, mtaalamu wa matumizi ya kompyuta
Na Henry Mwakifuna
Maisha ya sasa bila elimu si kitu. Hayo yamesemwa na Mwalimu Peter Magoda, mtaalamu wa matumizi ya kompyuta, alipokuwa akizungumza na Pambazuko FM katika Chuo cha Maendeleo Ifakara.
Amesema wakazi wa Bonde la Kilombero hawana muamko wa elimu, na amewataka wazazi pamoja na walezi kuamka na kuhimiza watoto wao kusoma.
Aidha, amebainisha kuwa wanafunzi wengi hutoka mbali, jambo linaloonyesha kiu ya maarifa na umuhimu wa elimu katika maendeleo ya jamii.
ametoa wito kwa wazazi na jamii kwa ujumla kuongeza ari ya elimu ili kufanikisha maendeleo ya kijamii na kiuchumi.

Baadhi ya wanafunzi wamesema kuwa kushiriki katika mafunzo mbalimbali kunawasaidia kujifunza vitu vipya na kutopoteza muda kwa mambo yasiyo na msingi.
Wamesema kuwa kompyuta inawasaidia kujifunza hata ukiwa mwenyewe na wakati mwingine kuhepuka udanganyifu kwa wanaowapa kazi.
