Pambazuko FM Radio
Pambazuko FM Radio
29 July 2026, 07:43

Jeshi la Polisi Mkoa wa Morogoro kupitia kitengo cha usalama barabarani limeendeleza kampeni ya kutoa elimu kwa wamiliki na madereva wa matrekta na power tiller wilayani Mlimba ili kumaliza kabisa tatizo la ajali za barabarani.
Na: Isidory Mtunda
Jeshi la polisi wilayani mkoa wa Morogoro kupitia kitengo chake cha usalama barabarani limeendelea na kampeni ya kutoa elimu kwa wamiliki na madereva wa matrekta na Power tiller katika halmashauri ya wilaya ya Mlimba baada ya kukamilisha zoezi hilo katika halmashauri ya mji wa Ifakara.

Akizungumza na wamiliki na madereva wa vyombo hivyo wa tarafa ya Mbingu, DTO Blandina Kasongwa amesema lengo la zoezi hilo ni kumaliza tatizo la ajali barabarani na sio kupunguza tu.
Naye Mkuu wa Kituo cha Polisi Mbingu, ASP Bertha Matiku, amewaasa wamiliki wa vyombo hivyo kuhakikisha wanaajiri madereva wanaokidhi vigezo na kukagua mizigo inayobebwa ili kuzuia hatari zinazoweza kujitokeza
Kwa upande wao, washiriki wa mafunzo hayo wamemuomba DTO na timu yake kupeleka mafunzo hayo katika tarafa hiyo ili madereva wengi waweze kushiriki na hatimaye kupata leseni.

Akijibu maombi ya wananchi hao, DTO Kasongwa amewashauri wale wote walio tayari kushiriki mafunzo hayo kujiorodheshe majina yao kisha kuwakabidhi kwa mkuu wa kituo au Diwani wa kata hiyo, Mheshimiwa Joseph Chrispin Msumaly, kwa ajili ya utekelezaji zaidi.