Pambazuko FM Radio

Kituo cha Polisi Ifakara ni chakavu-Dc Kyobya

7 February 2023, 2:49 pm

Na Kuruthum Mkata

Uchakavu wa Jengo na miundo mbinu mibovu ya umeme katika   Kituo cha Polisi cha Wilaya ya Kilombero kilichopo Ifakara ,imepelekea Mkuu wa Wilaya ya Kilombero wakili Dunstan Kyobya kuagiza kufanya marekebisho ikiwa ni pamoja na kupaka rangi na kurekebisha mifumo ya umeme katika jengo hilo.

Ametoa maagizo hayo baada ya   kufanya ziara ya kushtukiza katika kituo hicho ambapo amejionea hali hiyo na kuagiza yafanyike maboresho haraka iwezekanavyo.

Mkuu wa Wilaya ya Kilombero wakili Dunstan Kyoba akisisitza kituo hicho kufanyiwa maboresho

 Katika ziara hiyo pia alipata wasaa wa kuzungumza na mahabusu aliowakuta katika Kituo hicho,ambapo baadhi wamemweleza makosa waliyoyafanya ikiwemo wizi wa  mtoto  na kuoa mwanafunzi .

Mkuu wa Wilaya ya Kilombero Wakili Dunstan Kyobya akizungumza na Mahabusu{Picha na Kuruthum Mkata}
Mkuu wa Wilaya Wakili Dunstan Kyobya akiwahoji Mahabusu wa Kituo cha Polisi Ifakara