Pambazuko FM Radio

Tahadhari Ya Moto

24 August 2021, 8:29 am

Na Katalina Liombechi

Wakulima katika Wilaya ya Kilombero wametakiwa kuchukua Tahadhari ya kudhibiti Moto hasa kipindi hiki cha Maandalizi ya Mashamba ili Kuzuia kuchoma Rasilimali Za Misitu.

Picha Kutoka Maktaba

Idd Hassan Liwiga ni Mhifadhi wa Misitu kutoka Wakala wa Huduma za Misitu Wilaya ya Kilombero wakati akifanya mazungumzo na Redio Pambazuko fm Ofisini kwake.

Mhifadhi huyo amesema wakulima wanahimizwa kuchukua tahadhari ambazo ni pamoja na kuomba kibali kutoka Ofisi ya kijiji,kuwajulisha majirani zake ili nao wachukue Tahadhari pamoja na kuepuka kuchoma Mashamba kipindi cha upepo au jua linapokuwa kali.

Aidha ametaja njia mbadala ya kusafisha mashamba kwa kufyeka nyasi zinapokuwa mbichi ambazo inasaidia udogo kubaki kwenye uasilia na kupata mbolea pamoja na kusaidia viumbe hai kuendelea kuishi na kurutubisha ardhi.

Hata hivyo amesema kwa watu watakaobainika kuchoma moto katika Maeneo ya Hifadhi kwa kutochukua tahadhari watachukuliwa hatua za kisheria

Idd Hassan Liwiga ni Mhifadhi wa Misitu

Katika Hatua nyingine Liwiga amesema wanakabiliana na changamoto ya Wafugaji kulisha katika maeneo ya Hifadhi ambapo ameeleza kuwa nao wamekuwa wakiwachukulia hatua za kisharia.