Pambazuko FM Radio

Bionuai Hatarini kutokana na shughuli za Kibinadamu-Kilombero

2 May 2024, 7:08 pm

Shughuli za Kibinadamu  katika Bonde la Kilombero zimetajwa kuhatarisha uhifadhi wa Bionuai.

Mratibu kutoka Shirika la Association Mazingira amezitaja shughuli hizo wakati akizungumza Na Radio pambazuko Fm kutokana na Uwepo wa Watu wanaolima kwa kuhama hama na Kuandaa mashamba kwa kukata miti pamoja na kuchoma Mkaa kwa Matumizi ya Nishati.

Hata hivyo Nimejionea Shughuli zingine kama Uvuvi wa kutumia Neti na Kufua kando ya Mto Lumemo hali inayohatarisha Mazalia na uendelevu wa Samaki.