Pambazuko FM Radio

Jamii imetakiwa kutohusisha Majukwaa ya wanawake na Siasa

14 August 2023, 6:55 pm

Wanawake wa Kata ya Usangule wakiwa kwenye uzinduzi wa Jukwaa la uwezeshaji Kiuchumi{Picha na Kataliana Liombechi}

Jamii ya Kata ya Usangule Wilayani Malinyi wametakiwa kutohusisha Majukwaa ya wanawake na mambo ya kisiasa kwani majukwaa hayo yapo kwa ajili ya kuwawezesha wanawake kiuchumi

Na Katalina Liombechi

Wanawake wa Jukwaa la uwezeshwaji kiuchumi Kata ya Usangule Wilayani Malinyi wamesema Miongoni mwa Changamoto zinazowakabili ni pamoja Baadhi ya wana Jamii kuhusisha Shughuli za Jukwaa na Maswaala ya Kisiasa.

Akisoma Risala katika Hafla ya Uzinduzi wa Jukwaa Hilo Mtendaji wa Kata ya Usangule Bi Hellen George amesema kuwa watu wamekuwa na Mawazo hasi ya  kuwa Jukwaa hilo lipo kwa maslahi ya Chama Fulani hali ambayo inawapa ugumu katika Utekelezaji wa Majukumu ya Jukwaa.

Afisa Mtendaji wa Kata ya Usangule Bi Hellen George {Picha na Katalina Liombechi}

Aidha amezitaja changamoto zingine kuwa ni Ukosefu wa Mikopo kutoka Taasisi mbalimbali za Kifedha,Mtaji mdogo wa Jukwaa pamoja na ukosefu  wa jezi za Mpira.

Sauti ya Afisa Mtendaji kata ya Usangule Bi Hellen George

Nao Baadhi ya Wana Jukwaa hao akiwemo mwenyekiti Janeth Kamguna na Avelina Mwinami wamesema Uwepo wa Jukwaa hilo umewasaidia kuwaunganisha na Fursa mbalimbali za Kiuchumi,kufahamu namna ya kujitambua na kukumbushana mambo mbalimbali yahusuyo Afya Ndoa na Malezi.

sauti za badhi ya Wanajukwaa wakizungumza kwenye uzinduzi wa jukwaa hilo

Mgeni Rasmi katika Hafla hiyo Diwani wa Kata ya Usangule Mh Fadhili Liguguda amesema Watu waondoe dhana ya kuhusisha Jukwaa na Mambo ya Chama kwani Maudhui yake ni maalumu kwa akina mama wote pasi kujali Itikadi za vyama,Dini,wala kabila la Mtu.

Picha ya Diwani wa Kata ya Usangule Mh Fadhili Liguguda {Picha na Katalina Liombechi}
Sauti ya Diwani wa Kata ya Usangule Fadhili Liguguda akizungumza katika uzinduzi wa jukwaa la wanawake katika Kata hiyo

Hata hivyo akizungumzia Changamoto ya Mikopo Diwani huyo amesema Halmashauri imekuwa kitoa Mikopo ya Asilimia 4 Kwa Vikundi vya Wanawake wenye sifa lakini baadhi yao wamekuwa wagumu kufanya Marejesho.

Diwani Liguguda akizungumzia kuhusu Mikopo