Pambazuko FM Radio

TCCIA Kilombero inaenda kwa kusua sua

12 April 2023, 7:39 pm

Mwenyekiti wa TCCIA Wilaya ya Kilombero Bwana Samson Ngwila{Picha na Katalina Liombechi}

Wanachama wetu wanataka chama kiwasaidie na sio wakisaidie chama,wakipata fursa ya mikopo na wakamaliza mikopo hawaoni tena umuhimu wa chama,kwani wanachama wengi wakitatuliwa matatizo yao hawaonekani tena kwenye chama-Samson Ngwila

Na Elias Maganga

Wanachama wa Chama cha wafanyabiashara ,wenye viwanda na wakulima Wilayani Kilombero {TCCIA} wanaona umuhimu wa chama pale tu wanapopatwa na matatizo au kupatiwa fursa ya mikopo.

Hayo yameelezwa na Mwenyekiti wa Chama hicho Bwana Samson Ngwila alipokuwa akizungumza na Pambazukofm katika Kipindi cha Jioni leo.

Bwana Ngwila amesema wanachama wanaona umuhimu wa chama pale wanapopatwa na matatizo au pindi wanapopata fursa ya kukopa ndipo huwa wanakikimbilia chama na wanapomaliza mikopo, huwa hawana habari jambo linalopelekea kusua sua kwa chama hicho.

sauti ya samson ngwila akielezea kusua sua kwa chama

Bwana Ngwila amesema TCCIA ni chama cha wafanyabiashara,wenye viwanda na wakulima Tanzania,na kazi yake kubwa ni kuwajengea uwezo,kuwatetea na kutengeneza ushawishi kwa serikali kupata mapato.

Samson Ngwila akielezea kazi za TCCIA

Pamoja na kutekeleza hayo chama hicho kwa Wilaya ya Kilombero kimeonekana ni msaada mkubwa,ambapo kimewatetea wafanyabiashara waliotakiwa kuondolewa mjini na kupelekwa pembezoni.

Hata hivyo kwa sasa Chama hicho kinapambana kuhakikisha kinapata wanachama wengi ili kuimarisha umoja wao utakaowawezesha kutatua kero zinazowakabili.

Samson Ngwila akizungumzia changamoto walizozitatua kupitia chama hicho

Katika kutatua baadhi ya kero wanatarajia kukutana na Mkuu wa Wilaya ya Kilombero Bwana Dunstan Kyobya katika mkutano utakaowajumuisha wafanyabishara,wenye viwanda pamoja na wakulima  utakaofanyika April 11 Mwaka huu.

Sauti ya Mwenyekiti wa TCCIA akielezea mkutano