Pambazuko FM Radio

Andaeni mikakati ya usafi ili itekelezwe

19 February 2023, 4:13 pm

Na Rifati Jumanne

Katika kuhakikisha Halmashauri ya Mji wa Ifakara inarejea katika usafi wa mazingira,mashirika yasiyo ya kiserikali Wilayani Kilombero imewaomba Halmashauri ya Wilaya kuandaa mikakati maalumu ili wao waitekeleze kama ilivyo azma yao ya kusaidiana na serikali katika kila nyanja.

Halmashauri iandae mpango  mkakati na ugawanywe kwa Mashirika mbalimbali

Akizungumza katika Ofisi za Shirika la Uhifadhi wa wanyama Pori Afrika,Mwenyekiti wa mashirika yasiyokuwa ya kiserikali Wilayani humo Bwana Alexender Mpwaga amesema wao wako tayari kushirikiana na Halmashauri endapo watatimiza makubaliano ya kikao walichoketi hivi karibuni chakuwataka kuandaa mikakati ya utekelezaji wa uhifadhi wa taka ngumu na laini.

Mwenyekiti wa mashirika yasiyokuwa ya kiserikali Wilayani Kilombero Bwana Alexender Mpwaga{Picha na Rifat Jumanne}
Sauti ya Mwenyekiti wa mashirika yasiyokuwa ya kiserikali Wilayani Kilombero Bwana Alexender Mpwaga akielezea utayari waliono kusaidia na seriakli

Amesema kuna mashirika zaidi ya 13 anayoyasimamia yanajielekeza katika uhifadhi wa mazingira hivyo ni rahisi kama mikakati ikapatikana wao kugawana na kufanya utekelezaji kuwa rahisi na wa haraka ili kurejesha halmashauri katika hali ya usafi.

Akizungumzia kuhusu uhifadhi wa taka mwenyeketi huyo amesema kupitia shirika la uhifadhi wa wanyama pori Afrika tayari walishaanza kutoa elimu juu ya ujenzi na matumizi sahihi ya vizimba ambapo mpaka sasa tayari vizimba viwili vimeshajengwa wilayani Kilombero na kimoja kimejengwa kwa Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi.

Sauti ya Mwenyekiti wa mashirika yasiyokuwa ya kiserikali Wilayani Kilombero Bwana Alexender Mpwaga akizungumzia uhifadhi wa taka

Ikumbukwe hivi karibuni Halmashauri imeanzisha kampeni ya kufanya usafi yenye ujumbe wa “Mita tano usafi wangu.usafi wangu mita tano” ili kuhakikisha Halmashauri hiyo inarejea katika hali yake ya usafi.