Pambazuko FM Radio

Semina ya kuwawezesha wakulima kielimu ili kuongeza tija katika mazao

19 April 2024, 9:20 pm

Picha ni wakulima na wadau wa kilimo halmashauri ya mji wa Ifakara walioshiriki semina mjini Ifakara. Picha na; Isidory Mtunda

Wakulima wa halmaashauri ya mji wa Ifakara, wamepatiwa semina, ili waongeze tija katika kilimo, na kuacha kilimo cha mazooea , wakulima wengi halmashauri ya mji wa Ifakara, wakati mwengine wamekuwa wakilima bila kushirikisha maafisa ugani, kwa njia ya semina jamii inaweza kupata maarifa, ujuzi na nidhamu katika kilimo hatimaye kupata tija katika mazao.

Na; Isidory Mtunda

Zaidi ya wakulima 600 wa halmashauri ya mji wa Ifakara wilaya ya Kilombero mkoani Morogoro wamepatiwa mafunzo ya kilimo bora, udhibiti wa sumu kuvu na athari za mabadiliko ya tabia nchi.

Akizungumza na Pambazuko fm, meneja mauzo wa kampuni ya Hughes Agricultural Tanzania Ltd bwana Boniface Elias Molel amesema, semina hiyo inalenga kuwapa wakulima elimu ili kuboresha na kuongeza tija katika kilimo.

Meneja mauzo Boniface Molel – Picha na: Isidory Matandula

Sauti ya Meneja mauzo Boniface Molel

Naye afisa usalama wa chakula Mathias Mapesa kutoka wizara ya kilimo ametoa mada kuhusu sumu  kuvu, ambapo ametaja mazao yanayoshambuliwa na sumu hiyo kuwa ni pamoja na; mahindi, karanga mtama, alizeti Korosho na viungo.

wa kwanza kushoto Mathias Mapesa – Picha na Isidory Matandula

Sauti ya Mathias Mapesa

Aidha bwana Mapesa amesema moja ya madhara ya sumu kuvu ni kuzaa watoto wenye ulemavu wa viungo kama vile; mgongo wazi, mdomo sungura na au kuzaa mtoto asiye na sehemu ya haja kubwa.

sauti ya Mapesa

Kwa upande wao wakulima walioshiriki semina hiyo akiwepo; Josefina Liteleko, Agripina  Njowelo na Medard Nyachi wamejifunza namna ya kuhifadhi mazao ili  kuzuia sumu kuvu na matumizi sahihi ya mbolea.

Sauti za wakulima walioshiriki semina

Semina hiyo ni ya siku mbili, ambayo  ilifadhiliwa na kampuni ya Hughes Agricultural Tanzania Ltd, wauzaji na wasambazaji wa matrekta aina ya New Holland Agriculture, iliyofanyika katika ukumbi wa vijana mjini Ifakara mkoani Morogoro.