Pambazuko FM Radio

Tembo Wavamia Mashamba,Wala Mazao Ulanga

29 June 2021, 6:13 am

Na: Katalina Liombechi

Wakulima wa Mashamba ya Luhogi katika kata ya Minepa wamelalamikia Tembo kufanya uharibifu wa Mazao yao hali ambayo inaweza kuwapelekea kukumbwa na baa la njaa kwa Mwaka huu.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti wakulima hao akiwemo Costasia David,Athman Njelemela,Mwamini Juma Mwanga wamesema Tembo hao wamekuwa wakifanya uharibifu Mkubwa wa Mazao yao kiasi ambacho wengine watapata Mavuno hafifu na wengine kushindwa kabisa kuvuna licha ya kutumia gharama nyingi katika uhudumiaji.

Wamesema Mara nyingi wamekuwa wakiripoti changamoto hiyo kwa uongozi wa Kijiji cha Kivukoni nao kuwasilina na Uongozi wa Wilaya kwa ajili ya Udhibiti lakini inaonekana wameshindwa kuwadhibiti Tembo hao kwani wamekuwa wengi na mara nyingi anayekwenda kubiliana nao ni Mtu mmoja.

Hata hivyo Wakulima hao wameelezea wasiwasi wao kupata hasara katika Mavuno pamoja na kukosa chakula.

Costasia David,Athman Njelemela,Mwamini Juma Mwanga

Mwenyekiti wa Kijiji cha Kivukoni Shaneli Masasi amesema Malalamiko hayo yamekuwa yakiletwa na wakulima hao ambapo wamekuwa wakiwasiliana na Ofisi ya Maliasili nao kumwagiza Mtu kwa ajili ya kwenda kuwadhibiti.

Mwenyekiti Wa Kivukoni Shanel

Pambazuko FM imemtafuta Afisa wanyamapori Wilaya ya Ulanga Felisian Kisoma ambapo amekiri kupokea Malalamiko hayo na wamekuwa wakiyashughulikia kwa kuwaagiza Askari wa Wanyamapori kwenda mara kwa mara kuwadhibiti huku akieleza kuwa changamoto kubwa ni Uhaba wa Watumishi katika  Idara hiyo.

Aidha amesema Mashamba hayo yanapakana na Hifadhi hivyo imekuwa rahisi kwa Wanyama kutoka Hifadhini kwenda kwenye Mashamba ya Watu kufanya Uharibifu.

Hata hivyo ametoa wito kwa Wakulima wa Maeneo hayo kufanya Shughuli Rafiki kando ya maeneo ya Hifadhi kama vile Ufugaji wa Nyuki ambapo Wao wanajipanga na Wanaandaa Programu namna ya kutoa Elimu na kuhamasisha zaidi Ufugaji wa Nyuki Katika Eneo hilo.

Afisa wanyamapori Wilaya ya Ulanga Felisian Kisoma