Pambazuko FM Radio

AWF yakabidhi vifaa vya kusaidia uhifadhi wa mazingira vyenye thamani ya zaidi ya Sh mil 29

31 August 2023, 11:37 pm

Meneja wa AWF Clarence Msafiri (kushoto) akikabidhi Vifaa hivyo na Mtendaji wa Kata ya Vidunda Peter Lezile akipokea (Picha Katalina Liombechi)

Shirika linalojihusisha na uhifadhi wa Mazingira Afrika (AWF) limetoa vifaa hivyo ni katika Utekelezaji wa Mradi wa SUSTAIN_ECO Unaotekelezwa kwa Miaka Mitatu katika Halmashauri za Mji wa Ifakara,Mlimba na Wilaya ya Kilosa unaolenga kurejesha Mifumo Ikolojia kwa Maendeleo Endelevu.

Na; Katalina Liombechi – Ifakara

Vifaa vyenye thamani  Zaidi ya Sh Mil 29 vimetolewa na Shirika linalojihusisha na Uhifadhi wa Wanyamapori Afrika (AWF) kusaidia shughuli za Kiuchumi Rafiki kwa Mazingira katika Kata ya Vidunda Wilaya ya Kilosa na Tarafa ya Mngeta Halmashauri ya Mlimba Wilayani Kilombero.

Akizungumza wakati wa kukabidhi baadhi ya Vifaa hivyo katika Ofisi za kata ya Vidunda Meneja wa Shirika la AWF Clarence Msafiri amesema hiyo ni katika Utekelezaji wa Mradi wa SUSTAIN_ECO Unaotekelezwa kwa Miaka Mitatu katika Halmashauri za Mji wa Ifakara,Mlimba na Wilaya ya Kilosa unaolenga kurejesha Mifumo Ikolojia kwa Maendeleo Endelevu.

Amesema Msaada huo wa Vifaa unalenga kuunga Mkono juhudi za Wananchi wa Maeneo hayo kwa kuwa na dhamira ya Kufanya shughuli za Kiuchumi ambazo zitaboresha maisha yao kwa kujipatia kipato na kuacha kuharibu mazingira.

sauti ya Meneja AWF Clarence Msafiri

Mchumi Kilimo Alexanda Mpwaga na Mhifadhi kutoka AWF Antidius Raphael Wamesema Msukumo wa Kusaidia vifaa hivyo umekuja kutokana na kuona uhitaji wao na kuamua kuwapatia mafunzo ya Ujasiliamali na Kilimo Biashara katika kata ya Vidunda Kilosa na Tarafa ya Mngeta Halmashauri ya Mlimba ambapo Vikundi vitanufaika kwa kufanya shughuli za kilimo cha Miti ya Asili,matunda,Ufugaji wa Nyuki,Samaki na kuku Shughuli ambazo haziathili mazingira huku kwa Upande wa Kata ya Vidunda wanaamini Elimu hiyo inarithishwa kwa Wanafunzi wa Shule ya Msingi Vidunda kupitia kikundi cha Ufugaji wa Nyuki kilichopo katika shule hiyo

Aidha awali Wananchi hao wa Kata ya Vidunda walipatiwa Miche mbalimbali ya Matunda ikiwa ni pamoja na miche ya miembe 1500,Parachichi 1500 na Machungwa 600 ambapo Itakapokuwa itawasaidia kujipatia kipato na kuacha kufanya shughuli zinazoweza kuharibu mazingira na walitumia Fursa hiyo kuelezea uhitaji wa Vifaa vitakavyosaidia kurahisisha shughuli hizo za uhifadhi.


.

Mhifadhi AWF Antidius Raphael akiwakabidhi Miche Baadhi ya Wananchi wa Vidunda na kumweleza Mhifadhi uhitaji wa Vifaa (Picha kwa hisani ya AWF)

Sauti ya Mchumi Kilimo Mpwaga na Mhifadhi Antidius Raphael

Mpwaga amevitaja vifaa walivyokabidhi kusaidia shughuli hizo kuwa ni pamoja na Matoroli,Majembe,Reki ,Water keni ,viriba ,Gamboot ,Mikasi ya kupogolea ,Makoti ya Mvua ,Chepe ,vikinga vumbi na Sprayer za wadudu ambapo ameeleza kuwa vifaa kama hivyo pia vimetolewa katika Tarafa ya Mngeta Halmashauri ya Mlimba.

Mchumi Kilimo AWF Alexanda Mpwaga (Picha na Katalina Liombechi)

sauti ya Mchumi Kilimo Alexanda Mpwaga

Wakizungumza Mara baada ya Kupokea vifaa hivyo Mtendaji wa Kata ya Vidunda Peter Lezile na wananchi Janeth Nzagu na Mwenyekiti wa Kijiji cha vidunda Lazaro Kiboga wameshukuru kwa Msaada wa Vifaa hivyo ambavyo vitawasaidia kupata tija kupitia shughuli hizo na watajivunia kuhifadhi mazingira kwa Maendeleo endelevu.

Mwenyekiti wa Kijiji cha vidunda Lazaro Kiboga (Picha na Katalina Liombechi)

Sauti za Mtendaji wa Kata ya Vidunda Peter Lezile mwananchi Janeth Nzagu na Mwenyekiti wa Kijiji cha vidunda Lazaro Kiboga

Mradi wa SUSTAIN-ECO Unatekelezwa kwa Miaka 3 na Shirika la Uhifadhi wa Wanyamapori Afrika AWF kwa kushirikiana na Shirika la Umoja wa Mataifa la Uhifadhi wa Mazingira IUCN Mradi ambao unatekelezwa katika Halmashauri ya Mji wa Ifakara,Mlimba na Wilaya ya Kilosa na unafadhiliwa na Serikali ya SWEDEN.