Pambazuko FM Radio

Wanaushirika Kilombero wapatiwa mafunzo

26 April 2023, 2:46 pm

wanachama wa ushirika wa uvuvi,usindikaji na masoko wakifuatilia mafunzo{Picha na Elias Maganga}

Vyama vingi vya ushirika vimekufa kutokana na kutokuwa na elimu ya ushirika na kutokuwa na siri, hivyo wanachama wametakiwa kuitumia elimu waliyoipata ili kuundeleza ushirika huo

Na Elias Maganga

Wanachama wa chama cha ushirka cha Uvuvi ,usindikaji na masoko Wilaya ya Kilombero Mkoani Morogoro,wamepatiwa mafunzo ya dhana ya ushirika ,uongozi bora na uendeshaji wa chama cha ushirika

Mafunzo hayo yametolewa na Benk ya NMB  kupitia mwezeshaji  Thobias Mkamate ambaye ni Afisa Mafunzo wa Benki hiyo  ,amesema kuwa  lengo la kuwapatia mafunzo wanachama wa ushirika huo  ni kuufanya  kuwa imara,endelevu ili uweze kukopesheka kiurahisi

Afisa Mafunzo wa Benki ya NMB Thobias Mkamate akitoa mafunzo{Picha na Elias Maganga}

Sauti ya Afisa Mafunzo wa Benki ya NMB Thobias Mkamate

Akielezea misingi ya ushirika Bwana Mkamate amesema inazingatia maadili ambayo ni kujitegemea,uwajibikaji,demokrasia haki ,usawa na mshikamano.

Sauti ya Afisa Mafunzo wa Benki ya NMB Thobias Mkamate akielezea misingi ya Ushirika

Akishukuru kwa niaba ya wanachama wa chama cha ushirika uvuvi,usindikaji na masoko Kilombero ,mwenyekiti wa ushirika huo Bwana Abubakari Mashamba,amesema vyama vingi vya ushirika vimekufa kutokana na kutokuwa na elimu ya ushirika na kutokuwa na siri, hivyo amewaomba wanachama kuitumia elimu waliyoipata kuundeleza ushirika.

Hata hivyo Bwana Mashamba amewakaumbusha wanachama kulipa hisa na michango ya kila mwezi kama walivyokubaliana kwenye mkutano  uliyopita,kwani wanatarajia kuanza kukopeshana kwa ayule asiyechanga wala kununua hisa hatokopesheka

Mwenyekiti wa ushirika Bwana Abubakary Mashamba{Picha na Elias Maganga}

Sauti ya Mwenyekiti wa ushirika Bwana Abubakary Mashamba

Baadhi ya wajumbe waliohudhuria mafunzo hayo wamesema kupitia elimu waliyoipata watahakikisha wanaitumia ili ushirika huo usonge mbele kama malengo  ya chama chao kinavyojieleza.

Mwanachama wa chama chama ushirika Bwana Waziri chikula {Picha na Elias Maganga}

Sauti za baadhi ya wanachama wa ushirika