Pambazuko FM Radio

Kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi ni kubadili tabia-Kipindi

2 May 2024, 7:30 pm

Jamii imetakiwa kubadili tabia katika kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi ili kuzuia athari zitokanazo na uharibifu wa mazingira ya asili.

Afisa Mazingira kutoka Idara ya Mazingira na Maliasili Halmashauri ya Mji wa Ifakara Salome Mayenga ameyasema hayo wakati akizungumza na Pambazuko Fm kupitia kipindi Maalum kuhusu uhifadhi wa bionuai na mazingira kwa ujumla ambapo amesema shughuli za kibinadamu zimepelekea kubadili mazingira ya asili ambapo matokeo yake ni adha ya mvua zisizo na mpangilio yanayosababisha hali ya mafuriko.