Pambazuko FM Radio

Uhalifu Wapungua 75%,Wananchi waondolewa Hofu

18 May 2021, 5:36 am

Baadhi  ya  wananchi  wa  Mtaa wa Mangwale  Kata  ya viwanja sitini katika Halmashauri ya Mji wa Ifakara Wilayani Kilombero wameeleza  wasiwasi  wao  juu ya vitendo vya kiuhalifu vinavyotokea   kwenye mtaa huo.

Wakizungumza na pambazukofm baadhi ya wakazi hao akiwemo Joyce  Kaonja na Peter  Kinjara  wamesema vitendo vya uhalifu hususani wizi umekithiri katika mtaa huo  ambapo wamedai kuwa wizi huo umefanyika hasa katika kipindi cha masika.

Wakazi hao wa mtaa wa mangwale wamesema kuwa vitendo vya wizi vinarudisha nyuma maendeleo ya watu kwani mpaka sasa wamedai kuwa ni watu wengi waliolalamika  kuibiwa.

Mwenyekiti  wa mtaa  huo wa   Mangwale  Bwana Henrick  Ngulukila   amekiri kuwepo kwa  wizi katika mtaa huo na ameongeza kuwa jitahada za viongozi kwa kushirikiana na wananchi walifanikiwa kuwakamata baadhi ya wahalifu na kufikishwa kwenye vyombo vya sheria.

Bwana Ngulukila amesema kufuatia kukamatwa na kufungwa kwa wahalifu hao ,vitendo vya wizi vimepungua kwa asilimia 75 huku jitihada za kuendelea kuwasaka wezi zikiendelea.

Mwenyekiti  wa mtaa wa   Mangwale  Henrick  Ngulukila