Pambazuko FM Radio

Wadau wa Mazingira wakusudia kushirikisha Jamii utunzaji Endelevu wa Maliasili-Kilombero.

2 May 2024, 12:00 pm

Wadau wa Mazingira Bonde la Kilombero wakiwa kwenye kikao kazi {Picha na Katalina Liombechi}

Changamo za kibinadamu zinavyohatarisha usalama wa Maliasili Ikiwa ni pamoja na Kilimo holela,Ufugaji kwenye maeneo ya Hifadhi,Makazi holela na Utegemezi wa Rasilimali Zilizohifadhiwa kwani watu hukata miti kwa matumizi ya kuni na Mkaa Isivyo halali.

Na Katalina Liombechi

Katika kukabiliana na Uharibifu wa Maingira ya Asili Wadau wa wamekutana kujengeana Uwezo namna ya kushirikisha Jamii kuhifadhi Maliasili.

Haya yanakuja baada ya Wahifadhi na Wadau wa Mazingira Akiwemo Kamanda wa Pori la Akiba Kilombero Mhifadhi Bigilamungu Kagoma na Afisa Kilimo kutoka Mlimba kuelezea Changamo za kibinadamu zinavyohatarisha usalama wa Maliasili Ikiwa ni pamoja na Kilimo holela,Ufugaji kwenye maeneo ya Hifadhi,Makazi holela na Utegemezi wa Rasilimali Zilizohifadhiwa kwani watu hukata miti kwa matumizi ya kuni na Mkaa Isivyo halali.

Kamanda wa Pori la Akiba Kilombero Mhifadhi Bigilamungu Kagoma{Picha na Katalina Liombechi}
Sauti za wadau wa mazingira Kilombero

kwa Mujibu wa Mchumi Kilimo kutoka AWF Alexander Mpwaga Amesema lengo ni kujadili mbinu kuendeleza Ajenda za Kitaifa za Uhifadhi katika Mipango na bajeti za Serikali kusaidia usimamizi mzuri wa Maliasili.

Picha ya Mchumi Kilimo kutoka AWF Alexander Mpwaga{Picha na Katalina Liombechi}
Sauti ya Mchumi Kilimo kutoka AWF Alexander Mpwaga

Hata hivyo Baadhi ya Wadau waliohudhuria kikao kazi hicho Akiwemo Afisa Maliasili Kutoka Mkoa wa Morogoro Joseph Chuwa,Afisa Tarafa Ifakara Irene Shija na Mhifadhi Daraja la Kwanza kutoka TFS Shukrani Madinda wamesema kikao hicho kimewakumbusha Majukumu yao ili kufanya Shughuli za kiuchumi kuwa na Uendelevu.

Picha ya wadau wa Mazingira Bonde la Kilombero {Picha na Katalina Liombechi}
Sauti za wadau wa Mazingira Bonde la Kilombero

Kikao hicho Cha siku mbili Kilichoitwa na Mfuko wa Uhifadhi wa Wanyamapori Afrika AWF kimejumuisha Wataalam kutoka Sekta mbalimbali Halmashauri za Wilaya ya Kilosa,Mlimba, Mji wa Ifakara,Mkoa wa Morogoro na Taifa kimefanyika Ukumbi wa TTCIH Ifakara, kikilenga Kuzishusha Ajenda za Kitaifa za Utunzaji wa Mazingira kwa wananchi ili kuwe na Usimamizi mzuri wa Maliasili.