Pambazuko FM Radio

Wanusurika kifo baada ya nyumba yao kubomoka-Ifakara

1 April 2024, 2:30 pm

Picha ya Nyumba ya Bwana Aron Nyoni iliyoanguka {Picha na Elias Maganga}

Hakuna kifo wala majeruhi kutokana na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha baada ya nyumba kubomoka ambayo imeacha familia ya watu watatu kukosa makazi,ambapo kwa sasa wamehifadhiwa katika Jengo la Ccm kata ya Kibaoni katika Halmashauri ya Mji wa Ifakara“-Afisa Mtendaji wa Kijiji cha Kikwawila Bwana Gregory Midas.

Na Elias Maganga

Baba na watoto wake wawili wamenusurika kifo baada nyumba waliyokuwa wamelala kuanguka kutokana na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha katika Halmashauri ya Mji wa Ifakara Wilayani Kilombero.

Akizungumza na Pambazukofm, Afisa Mtendaji wa Kijiji cha Kikwawila Bwana Gregory Midas amesema tukio hilo limetokea usiku wa march 31 kuamkia April Mosi mwaka huu.

Bwana Midas amesema nyumba iliyoanguka ni ya bwana Aron Nyoni, na ni ya chumba kimoja ambapo kuta zake zimeanguka kwa nje na kufanikiwa baba na wanae  kutoka wakiwa salama na kwasasa wamepewa hifadhi kwenye jengo la chama cha mapinduzi ccm Kata ya Kibaoni.

Sauti ya Afisa Mtendaji wa Kijiji cha Kikwawila Bwana Gregory Midas