Pambazuko FM Radio

Biashara hewa ukaa kukabiliana na tabianchi bonde la Kilombero

30 April 2026, 18:53

Picha inayoonyesha zoezi la utiaji saini biashara ya hewa ukaa(Picha na Kuruthumu Mkata)

Mradi huo utasaidia kurejesha maeneo yaliyoharibika, kulinda mazingira na kuinua kipato cha wananchi, huku ukitarajiwa pia kutoa manufaa ya kijamii

Na Kuruthumu Mkata

Kampuni ya Lasting Forest Solutions imesaini hati ya makubaliano ya biashara ya hewa ukaa na Jumuiya ya Uhifadhi wa Wanyamapori ya ILUMA, hatua inayolenga kuhifadhi mazingira na kukabiliana na changamoto za mabadiliko ya tabianchi.

Akizungumza leo April 30, 2026 katika hafla ya kusaini makubaliano hayo Mkurugenzi wa kampuni hiyo, Dkt.Hamidu Ami Seki, amesema mradi huo utasaidia kurejesha maeneo yaliyoharibika, kulinda mazingira na kuinua kipato cha wananchi, huku ukitarajiwa pia kutoa manufaa ya kijamii ikiwemo madawati na mafunzo ya wataalamu wa ndani.

Picha ya Dkt.Hamidu Ami Seki Mkurugenzi wa Lasting Forest Solutions(Picha na Kuruthumu Mkata)
Sauti ya Dkt.Hamidu Ami Seki Mkurugenzi wa Lasting Forest Solutions

Mkuu wa Wilaya ya Kilombero, Dunstan Kyobya, amesema makubaliano hayo ni hatua ya awali kuelekea mkataba kamili, akisisitiza umuhimu wa usimamizi wa kisheria.

Picha ya Mkuu wa Wilaya ya Kilombero(Picha na Kuruthumu Mkata)
Sauti ya Mkuu wa Wilaya ya Kilombero

Naye katibu wa ILUMA abubakary mbongile amesema ujio wa mradi huo ni faida kwa hifadhi ya iluma na wananchi wake ambapo ameeleza kupitia makubaliano ya awali ambayo yatadumu kwa miezi sita wataalam watapelekwa kwenye mafunzo ya hewa ukaa na kuanzishwa kwa vikundi mbalimbali katika vijiji vilivyopitiwa na hifadhi hiyo.

Sauti ya Katibu Jumuiya ya Hifadhi ya ILUMA

Viongozi wa baadhi ya vijiji vinavyopitiwa na mradi huo wameeleza matarajio yao na namna wananchi watakavyonufaika  kiuhifadhi na maendeleo ya jamii.

Sauti za Wenyeviti

Hafla ya kusaini makubaliano hayo ya biashara ya hewa ukaa imefanyika Katika Halmashauri ya Mji wa Ifakara Wilayani Kilombero na kushuhudiwa na wakuu wa wilaya Za Kilombero na Ulanga,wakurugenzi wa Halmashauri hizo mbili,wanasheria na wadau wengine muhimu katika maeneo hayo ya mradi.