Pambazuko FM Radio

Sekiboko: Mabinti msikate tamaa, rejeeni kutimiza ndoto zenu

2 August 2026, 18:20

Picha ya mabinti waliokatisha masomo au kukata tamaa kutokana na changamoto za ujauzito kutoka Taasisi ya Enlight Development Organization (EDO) (Pcha na Henry Mwakifuna.)

Mheshimiwa Sekiboko ameipongeza EDO kwa mchango wake katika kuwawezesha mabinti na wanawake waliopitia changamoto mbalimbali kurejea katika mkondo wa maendeleo kupitia elimu ya stadi za maisha, ushauri nasaha na programu za uwezeshaji wa kiuchumi.

Na Henry Mwakifuna

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Elimu, Mheshimiwa Husna Sekiboko, amewataka mabinti waliokatisha masomo au kukata tamaa kutokana na changamoto za ujauzito kutoruhusu mazingira hayo yazime ndoto zao, badala yake wajiamini, wajitambue na wachangamkie fursa zilizopo ili kujenga maisha yenye matumaini na mafanikio.

Akizungumza baada ya kutembelea Taasisi ya Enlight Development Organization (EDO) mjini Ifakara, wilayani Kilombero, Mheshimiwa Sekiboko ameipongeza taasisi hiyo kwa mchango wake katika kuwawezesha mabinti na wanawake waliopitia changamoto mbalimbali kurejea katika mkondo wa maendeleo kupitia elimu ya stadi za maisha, ushauri nasaha na programu za uwezeshaji wa kiuchumi.

Sauti ya mwandishi Henry Mwakifuna