Pambazuko FM Radio

Wadau Kilombero,Kilosa kusimamia udhibiti wa taka hatarishi kupitia vizimba

30 September 2026, 12:37

Wadau wa udhibiti wa taka hatarishi kupitia vizimba kutoka wilaya za Kilombero na Kilosa. Picha na Amina Mrisho

Taka hatarishi zinapotupwa hovyo zinaweza kuhatarisha afya za binadamu na kuchafua mazingira. Ili kukabiliana na changamoto hiyo, matumizi ya vizimba maalum ni miongoni mwa njia za kudhibiti na kuhifadhi taka hizo.

Na Amina Mrisho

Wadau mbalimbali kutoka Wilaya za Kilombero na Kilosa wamekutana kujadili namna bora ya kuimarisha udhibiti na usimamizi wa taka hatarishi kwa lengo la kulinda afya za wananchi, mazingira na kuhimiza matumizi ya vizimba kwa ajili ya kukusanya na kuhifadhi taka hizi.

Kikao hicho kilichoandaliwa na shirika la uhifadhi wa mazingira, kulinda viumbe hai, na kukuza maendeleo endelevu (IUCN) kiliwakutanisha wadau na viongozi mbalimbali wa Serikali, watendaji,vyama vya ushirika pamoja na wakulima wa miwa na mpunga.

Mkuu wa wilaya ya Kilombero wakili Dunstun Kyobya akiwa katika kikao na wadau wa udhibidi wa taka hatarishi kwa kutumia vizimba. Picha na Amina Mrisho

Akizungumza katika mkutano huo mkuu wa wilaya ya Kilombero Wakili Dunstun Kyobya amesema  matumizi ya vizimba vya kuwekea taka hatarishi ni muhimu kwa kuwa taka hizo zinaweza kusababisha madhara kwa afya ya binadamu na mazingira na kuongeza kuwa usimamizi wa taka hatarishi na matumizi sahihi ya vizimba unahitaji ushirikiano wa wadau wote hivyo amewataka viongozi kuanzia ngazi ya kijiji kutoa elimu kwa wananchi na kuwachukulia hatua watakaokiuka utaratibu watakaojiwekea.

Sauti ya mkuu wa wilaya ya Kilombero wakili Dunstun Kyobya

Kwa upande wake Said Kibwana mwenyekiti wa chama cha msingi Ilundo matambiko Amcoss (ILUMATA) amesema wao waliupokea vizuri mradi wa udhibiti wa taka hatarishi kupitia vizimba kwa kushirikisha jamii na kupata ushrikiano mzuri.

Sauti ya mwenyekiti wa ILUMATA AMCOS Said Kibwana

Aidha, wadau wamejadili mikakati madhubuti ya kuhakikisha Wilaya ya Kilombero na Kilosa zinakuwa na mfumo salama na endelevu wa usimamizi wa taka hatarishi.

Sauti ya Mdau

Kikao hicho kilihitimishwa kwa msisitizo wa kuimarisha ushirikiano, kuongeza uelewa wa jamii na kuhakikisha hatua stahiki zinachukuliwa katika kila hatua ya usimamizi wa na udhibidi wa taka hatarishi kupitia vizimba.

Mfano wa vizimba vya kuhifadhia taka hatarishi. Picha na IUCN