Pambazuko FM Radio
Pambazuko FM Radio
12 November 2026, 16:56

Huo ni uvamizi waondolewe wale wote waliovamia na kupora maeneo ya Halmashauri hii kutoka halmashauri nyingine mijadala ifuate baada ya kuwa nje ya eneo-Wakili Dunstan Kyobya.
Na Henry Mwakifuna
Mkuu wa Wilaya ya Kilombero, Wakili Dunstan Kyobya, amemuagiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mlimba kuhakikisha maeneo yote ya Halmashauri hiyo yaliyovamiwa na kutwaliwa na Halmashauri nyingine yanarejeshwa.
Akizungumza katika Baraza la Madiwani la Halmashauri hiyo, Kyobya amesema suluhu ya mgogoro huo ni waliovamia maeneo hayo kuondoka ili Halmashauri ya Mlimba irejeshewe maeneo yake.

Wakili Dunstan Kyobya Mkuu wa Wilaya ya Kilombero akizungumza na Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya Mlimba kwenye Kikao cha Baraza hilo Picha na Henry Mwakifuna
sauti ya DC Kyobya
Awali, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mlimba Martha Mkula alimuomba Mkuu wa Wilaya ya Kilombero kuingilia kati suala la baadhi ya maeneo ya Halmashauri hiyo yaliyoporwa na kutumiwa na Halmashauri nyingine, ili yaweze kurejeshwa.

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mlimba Mheshimiwa Martha Mkula akizungumza Kwenye Kikao cha Baraza la Madiwani