Pambazuko FM Radio
Pambazuko FM Radio
26 November 2026, 11:44

Gharama za dawa zimekuwa zikiongezeka mara kwa mara mfano ununuzi wa dawa,kumuona daktari,vipimo pamoja na kumuona daktari
Na Kuruthumu Mkata
Wananchi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mlimba wameiomba Serikali kupunguza gharama za matibabu katika vituo vya afya, wakieleza kumekuwa na kuongezeka kwa gharama siku hadi siku ambazo zimeendelea kuwa mzigo kwa wananchi.
Akizungumza katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika viwanja vya Shule ya Msingi Lukolongo, mbele ya Waziri Mkuu Dkt. Mwigulu Nchemba, mkazi wa Kata ya Mchombe amesema gharama za dawa zimekuwa zikiongezeka akitolea mfano gharama za ununuzi wa dawa, kumuona daktari na vipimo pamoja na kumuona daktari.
Akijibu hoja hiyo, Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Mlimba Nicholaus Semngoa amesema kwa sasa malipo ya huduma za afya yanafanyika kwa kutumia namba ya malipo (Control Number), akieleza kuwa mfumo huo una makato kidogo Huku akisema kuwa kila mgonjwa anapaswa kwanza kumuona daktari ili kubaini tatizo lake kabla ya kupewa huduma nyingine.

Akitoa maelekezo katika mkutano huo, Waziri Mkuu Dkt. Mwigulu Nchemba amesema Serikali kupitia Wizara ya Afya na Ofisi ya Rais – TAMISEMI itakaa pamoja na kujadili changamoto hiyo ili kuona namna bora ya kupunguza gharama za huduma za matibabu kwa wananchi.
