Pambazuko FM Radio
Pambazuko FM Radio
4 November 2026, 15:55

Hospitali ya Ifakara
Wenza wanahimizwa kuanza kwa vitendo kwa kugawana majukumu ya nyumbani, kusikilizana na kuheshimiana, ili kujenga familia zenye upendo, mshikamano na amani, na kulinda afya ya akili ya kila mmoja-Mwanasaikolojia
Na Nicolatha Mpaka
Wenza wamehimizwa kushirikiana katika kutekeleza majukumu ya kifamilia ili kuimarisha upendo, mshikamano na amani, pamoja na kuzuia changamoto za afya ya akili zinazoweza kujitokeza kutokana na kutokuwepo kwa ushirikiano.

Mwanasaikolojia Willison Mgaya kutoka kitengo cha Afya ya Akili Hospitali ya Rufaa ya Mkoa ya Mtakatifu Fransisco Ufakara Picha na Nicolatha Mpaka
Akizungumza na mwanahabari wetu, mwanasaikolojia Willison Mgaya amesema kutoshirikiana katika majukumu ya nyumbani kunaweza kusababisha migogoro, msongo wa mawazo na kudhoofika kwa mahusiano ya kifamilia.
Amesisitiza umuhimu wa wenza kupanga na kugawana majukumu ya nyumbani kwa kuzingatia uwezo na mazingira yao, huku wakijenga utamaduni wa mawasiliano, kuheshimiana na kusaidiana.
sauti ya Mwanasaikolojia
Wenza wanahimizwa kuanza kwa vitendo kwa kugawana majukumu ya nyumbani, kusikilizana na kuheshimiana, ili kujenga familia zenye upendo, mshikamano na amani, na kulinda afya ya akili ya kila mmoja.