Pambazuko FM Radio
Pambazuko FM Radio
10 October 2026, 16:40
vijana wamepewa elimu kuhusu afya ya uzazi na njia za kujikinga na ukatili wa kijinsia, ambapo mdahalo umeasaidia kuwapa nafasi ya kufafanuliwa na kuwa na uelewa zaidi-Mwalimu Makata

Afisa Utamaduni wa Halmashauri ya Mlimba Mwalimu Makata akizungumza wakati wa Bonanza hilo Picha na Kuruthum Mkata
Na Kuruthum Mkata
Halmashauri ya Wilaya ya Mlimba, kwa kushirikiana na Mradi wa HER Future unaotekelezwa na Pathfinder International kwa ushirikiano na Amani Girls Organisation (AGO), imeandaa bonanza la michezo na mdahalo wa vijana kwa lengo la kutoa elimu kuhusu afya ya uzazi na kupinga ukatili wa kijinsia.
Bonanza hilo lililofanyika katika Halmashauri ya Wilaya ya Mlimba limewashirikisha zaidi ya vijana 1,000, wataalamu wa maendeleo ya vijana kutoka Ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri, pamoja na viongozi wa kata na mitaa.
Afisa Utamaduni wa Halmashauri hiyo, Mwalimu Makata, amesema vijana walipata elimu kuhusu afya ya uzazi na njia za kujikinga na ukatili wa kijinsia, huku mdahalo ukiwapa nafasi ya kuuliza maswali na kupata ufafanuzi kutoka kwa wataalamu.
Sauti ya Mwalimu Makata
Baadhi ya vijana walioshiriki katika bonanza hilo wameipongeza Halmashauri ya Wilaya ya Mlimba na wadau wake kwa kuandaa shughuli hiyo, wakisema imewaongezea uelewa kuhusu afya ya uzazi, haki zao na namna ya kujikinga na ukatili wa kijinsia.
Halmashauri ya Wilaya ya Mlimba imesema itaendelea kushirikiana na Mradi wa HER Future pamoja na wadau wengine kuhakikisha vijana, wakiwemo watu wenye ulemavu, wanapata elimu na huduma muhimu za afya ya uzazi, pamoja na taarifa kuhusu namna ya kuzuia na kukabiliana na ukatili wa kijinsia.