Pambazuko FM Radio
Pambazuko FM Radio
28 October 2026, 18:25

Mkuu wa Wilaya ya Kilombero Wakili Dunstan Kyobya (katikati) akiwa na Meneja Mhusiano wa Kampuni ya Kilombero Victor Byemelwa (Kushoto) na Masista wa Upendo Picha na Kuruthum Mkata
Tunafurahi kuungana na Kituo cha Masista wa Upendo Ifakara katika suala la upendo katika mashirikiano na Taasisi mbalimbali tunaunga mkono Juhudi zao katika kutatua changamoto za jamii-Victor Byemelwa
Na Kuruthum Mkata
Kampuni ya Sukari Kilombero imekabidhi tani nne za sukari katika Kituo cha masista Upendo Mjini Ifakara kati ya tani nane zinazohitajika.
Akizungumza katika hafla hiyo, Meneja wa Mahusiano na Mawasilino kampuni Victor Byemelwa amesema wanaendelea kusaidia makundi mbalimbali yenye mahitaji maalumu kupitia uwajibikaji kwa jamii Ambapo Amesema hadi sasa kampuni imekabidhi tani kumi kati ya tani 23 zilizoahidiwa kwa taasisi na makundi mbalimbali, huku akimshukuru Mkuu wa Wilaya ya Kilombero kwa ushirikiano wake.
sauti ya Meneja wa Mahusiano na Mawasilino kampuni Victor Byemelwa

Mkuu wa Wilaya ya Kilombero, Wakili Dunstan Kyobya (Kulia) akizungumza na Wanahabari mara baada ya Kukabidhi Msaada huo Picha na Kuruthum Mkata
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Kilombero, Wakili Dunstan Kyobya, ameipongeza kampuni hiyo kwa kuendelea kusaidia jamii kupitia misaada mbalimbali huku Akisema Kituo cha Upendo kimetoa huduma kwa makundi mbalimbali kwa miaka 25, huku akiitaka taasisi na kampuni nyingine kuiga mfano huo.
sauti ya DC Kyobya
Naye Sista Raymunda Mgaya kutoka Kituo cha Upendo amewashukuru kampuni ya Kilombero Sukari kwa msaada huo unaosaidia kuendeleza huduma za kituo hicho pia Amesema kituo hicho hutoa mikate bure kwa watu 1,559 katika wilaya za Kilombero na Ulanga, pamoja na kusaidia hospitali, shule na makundi mengine yenye uhitaji.
sauti ya Sista Raymunda
Nao baadhi ya wanufaika na msaada huo akiwemo David Nyaluke na Ivodia Makawa kutoka Kituo cha Nazareti,wameishukuru kampuni hiyo kwa kusaidia upatikanaji wa mahitaji muhimu, ikiwemo huduma kwa wagonjwa huku Wakiziomba kampuni na taasisi nyingine kuiga mfano huo kwa kutoa misaada itakayoboresha maisha ya watu wenye mahitaji mbalimbali.
Sauti ya Wanufaika