Pambazuko FM Radio

Wananchi Mavimba wawasamehe kamati kwa mapungufu

5 October 2026, 17:55

hali hiii hapa tumepigwa kuna ubadhilifu hapaaaaa-mwananchi

Na Elias Maganga

Wananchi wa Kijiji cha Mavimba, Kata ya Milola  Halmashauri ya Wilaya ya Ulanga, wameisamehe Kamati ya Usimamizi wa Ujenzi wa Uzio wa Mnada wa Mavimba baada ya kubainika mapungufu kadhaa katika taarifa ya mapato na matumizi iliyowasilishwa kwenye mkutano wa kijiji uliofanyika october 2 mwaka huu Kijijini hapo.

Miongoni mwa mapungufu yaliyobainika ni taarifa kuonyesha kuwa miti milunda 700 ilinunuliwa wakati idadi iliyonunuliwa ni 533. Pia kulikuwa na hitilafu katika hesabu za ununuzi wa mabati saba ya geji 28, ambapo taarifa ilionyesha manunuzi  ya shilingi 366,000 badala ya shilingi 266,000.

sauti ya Baadhi ya Wananchi wa Mavimba

akitoa ufafanuzi mjumbe mmoja wapo ametaja malipo ya ushuru, upakizaji yamechangia kuwapo kwa Hesabu iliyopatikana

sauti ya Mjumbe wa kamati

Baada ya mjadala wa wananchi, mkutano uliazimia kwa kauli moja kuisamehe kamati hiyo huku ukiwataka wahusika kuhakikisha makosa kama hayo hayajirudii tena.

Akizungumza katika mkutano huo, Diwani wa Kata ya Milola, Masudi Kilala Ngongono, aliwapongeza wananchi kwa kufuatilia na kuhoji utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika kijiji chao, akisema ushiriki wao unasaidia kuimarisha uwajibikaji na matumizi sahihi ya rasilimali za umma.

Insert Diwani