Pambazuko FM Radio
Pambazuko FM Radio
3 November 2026, 14:49

Baadhi ya Wananchi wa Msolwa Station Halmashauri ya Ifakara Mji wakipunga mikono katika Mkutano wa hadhara mbele ya Mkuu wa Wilaya ya Kilombero Wakili Dunstan Kyobya Picha na Kuruthum Mkata
sisi kama vijana wa Msolwa Station Tunahitaji kupewa kipaumbele katika fursa mbalimbali za Kiuchumi ikiwemo Mikopo, kuwa mbali na barabara kubwa isiwe kikwazo cha kukosa Fursa-Mwakilishi Vijana.
Na Kuruthum Mkata
Vijana wa Kata ya Msolwa Station, Halmashauri ya Mji wa Ifakara, wameiomba Serikali kuweka kipaumbele katika kuwapatia fursa mbalimbali za kiuchumi, ikiwemo mikopo, ili waweze kujikwamua kiuchumi.
Akizungumza katika mkutano wa hadhara mbele ya Mkuu wa Wilaya ya Kilombero, Wakili Dunstan Kyobya, kijana Harun Rashid amesema vijana wanakabiliwa na changamoto katika mchakato wa kuomba mikopo, hususan wakati wa kuwasilisha maombi ya vikundi.
sauti ya Mwakilishi wa Vijana

Afisa Maendeleo ya Jamii wa Halmashauri ya Mji wa Ifakara Bi Florence Mwambene akitoa ufafanuzi katika mkutano wa Hadhara picha na Kuruthum Mkata
Kwa upande wake Afisa Maendeleo ya Jamii wa Halmashauri ya Mji wa Ifakara Bi Florence Mwambene amesema Kata ya Msolwa Station imetoa mikopo ya shilingi milioni 13, huku akitaja changamoto ya vikundi kuchelewesha marejesho na kuahidi kuendelea kutoa elimu na kufuatilia ulipaji wa mikopo.
sauti ya Afisa Maendeleo

Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Ifakara, Rashid Semgoya, akizungumza na Wananchi wa Kata ya Msolwa Station picha na Kuruthum Mkata
Naye Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Ifakara, Rashid Semgoya, amesisitiza vikundi kurejesha mikopo kwa wakati ili wengine wanufaike, huku akiahidi kutuma wataalamu ndani ya wiki moja kuwasaidia vijana waliokidhi vigezo lakini hawajapata mikopo, ikiwemo vikundi vya bodaboda.
sauti ya Kaimu Mkurugenzi

Wakili Dunstan Kyobya , Mkuu wa Wilaya ya Kilombero akitoa maagizo katika mkutano wa hadhara kata ya Msolwa Station picha na Kuruthum Mkata
Aidha Mkuu wa Wilaya ya Kilombero, Wakili Dunstan Kyobya,akijibu changamoto hiyo mbele ya mkutano wa hadhara amemuagiza Mkurugenzi kuhakikisha dirisha la mikopo linafunguliwa ili vijana wanufaike na fursa hizo, huku akisisitiza umuhimu wa kutoa elimu kuhusu mikopo mbalimbali inayotolewa na Serikali.