Pambazuko FM Radio
Pambazuko FM Radio
19 September 2026, 13:57
Msingi wa sekondari ni kiingereza katika kikisikiliza, kukisoma, kukitamka na kukiandika

baadhi ya Wanafunzi wa kozi ya kiingereza wanaojianda ana kidato cha kwanza picha Martin Mianjam
Na Henry Mwakifuna
Wazazi Wilayani Kilombero wamekumbushwa kuwapeleka watoto wao waliomaliza Darasa la Saba katika vituo vya maandalizi ya Lugha ya Kiingereza, ili kuwasaidia kukabiliana na changamoto ya uelewa wa lugha hiyo wanapoingia Kidato cha Kwanza.
Mianjam Martin, Mwalimu wa Lugha mbalimbali katika Mji wa Ifakara, amesema msingi wa elimu ya sekondari unatumia zaidi Lugha ya Kiingereza, hivyo wazazi na walezi hawana budi kuwapeleka watoto wao katika vituo vinavyofundisha lugha hiyo.

Mwalimu wa Lugha Martin Mianjam akizungumza na Mwandishi wa Taarifa hii picha na Henry Mwakifuna
Akizungumza katika Kipindi cha Asubuhi Mseto kinachorushwa na Pambazuko FM, amesema ni muhimu kuhakikisha mwanafunzi anajenga msingi mzuri wa Lugha ya Kiingereza ili kurahisisha maendeleo yake ya kielimu.
sauti ya Mwalimu wa Lugha Martin Mianjam
Baadhi ya wanafunzi waliosoma Lugha ya Kiingereza Nasma Mkwati na Innosencia Ngadaya wamesema kuwa kujifunza lugha hiyo tangu awali ni msingi mzuri unaowasaidia kurahisisha uelewa wa masomo wanapoendelea na elimu ya sekondari.
sauti ya baadhi ya Wanafunzi