Pambazuko FM Radio

Hapi akemea tabia ya kuwatekeleza watoto

13 August 2026, 13:18

Picha ya wanachama wa CCM Ifakara Wakiwa kwenye Mkitano wa Hadhara katika ofisi za CCM Kilombero. Picha Kuruthum Mkata

Vijana mnapaswa kuwajibika na msikwepe majukumu ya kulea watoto kwa kuwaachia wanawake mzigo wote wa kulea watoto

Na Kuruthum Mkata

Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Wazazi CCM Taifa na MNEC, Ally Hapi, amekemea tabia ya baadhi ya vijana wa kiume kuwapa mimba Mabint wadogo na baadaye kukwepa majukumu ya malezi ya watoto wao.

Hapi ameyasema hayo alipotembelea Shirika la Enlight Development Organization (EDO) linalowasaidia wamama wadogo kujikwamua kiuchumi kupitia kilimo na ujasiliamali, ambapo Amesema vijana wanapaswa kuwajibika na kuacha kuwaachia wanawake mzigo wote wa kulea watoto.

Pia amewataka wazazi na walezi kuendelea kuwafundisha vijana maadili ili kupunguza vitendo vya kutelekeza watoto na kuonya kuwa tabia hiyo inaweza kusababisha migogoro ya kifamilia na kuathiri amani katika jamii.

Picha ya Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Wazazi CCM Taifa Ndugu Ally Hapi, (picha na Kuruthum Mkata )
Sauti ya Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Wazazi CCM Taifa , Ally Hapi.

Kwa upande wake Mkurugenzi  Mwenza wa EDO Bi.Josephine Said amesema Shirika hilo linaendelea kuwawezesha wamama Wadogo kwa mafunzo ya ujasiriamali, ushonaji na kilimo cha mbogamboga ili kujikwamua kiuchumi.

Picha ya Mkurugenzi  Mwenza wa EDO Bi.Josephine Said akiwa na mama wadogo.
Sauti ya Mkurugenzi  Mwenza wa EDO Bi.Josephine Said

Naye Janet Mkongowele, mmoja wa wanufaika wa EDO, amesema kupitia mafunzo hayo wamefanikiwa kujikwamua kiuchumi na kuanza kujitegemea pia Ameishukuru EDO na viongozi mbalimbali kwa kuwapa msaada na kuwajengea matumaini mapya ya maisha.

Picha ya Baadhi ya wanufaika kutoka EDO (picha na Kuruthum Mkata)

Sauti ya Janet Mkongowele,