Pambazuko FM Radio
Pambazuko FM Radio
15 September 2026, 16:16

teknolojia mpya yapaswa kuendana na mabadiliko ya waandishi na watangazaji.
Na Henry Mwakifuna
Waandishi wa habari na watangazaji wa redio za jamii nchini wametakiwa kubadilika na kuendana na maendeleo ya teknolojia, hususan kila zinapotolewa teknolojia na mifumo mipya.
Akizungumza katika mafunzo kuhusu teknolojia ya Porto na maendeleo ya programu mbalimbali za App, mkufunzi kutoka Vikes, Makku Luikkonen, amesema mabadiliko ya teknolojia yanapaswa kwenda sambamba na mabadiliko ya mahitaji na matumizi ya watumiaji.
Amesema maendeleo na maboresho ya Porto pamoja na programu mbalimbali yataendelea kuunganisha vitu mbalimbali, huku matumizi ya sauti yakitarajiwa kuchukua nafasi muhimu zaidi sambamba na maandishi.

Awali, mkufunzi Hilali Ruhindwa ambaye ni mhariri mkuuu wa mtandao wa Redio Jamiii amewakumbusha waandishi na watangazaji kujikita katika maudhui yenye malengo mahususi, akitaja masuala ya mazingira, jinsi na mabadiliko ya tabianchi kuwa miongoni mwa maeneo yanayopaswa kupewa kipaumbele.
Baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo Furahini Sella wa Triple A fm na Epiphanus Danford wamesema kuwa mafunzo hayo yatawasaidia kuboresha utendaji wao wa kazi kwa Wanaoshiriki kwa mara ya kwanza na kuimarisha utendaji kwa waliyopata mafunzo kwa mara ya pili lakini yakijaziliza mafunzo ya Habari kwa watu wenye Ulemavu.

baadhi ya waandishi na watangazaji walioshiriki mafunzo juu ya Porto picha na Amua Rushita