Pambazuko FM Radio

DC Kyobya atoa onyo kwa wafugaji

19 August 2026, 13:19

DC Kyobya akisisitiza jambo (mwenye microphone) – picha na: Kuruthum Mkata

Mkuu wa wilaya ya Kilombero, wakili Dunstan Kyobya, ametoa onyo kali kwa wafugaji wanaochochea migogoro ya ardhi inayotishia amani na kusababisha vifo, akiwemo mkasa wa hivi karibuni wa Afisa Ardhi Ifakara. Wakati huohuo, Kaimu Mkurugenzi wa mji huo, Dk. Yuda Mgeni, amewasilisha changamoto zinazowakabili wafugaji zikiwemo migogoro na uhaba wa miundombinu kama majosho na masoko ya mifugo.

Na: Kuruthum Mkata

Mkuu wa Wilaya ya Kilombero, Wakili Dunstan Kyobya, amekemea vikali migogoro ya ardhi inayochochea vurugu na kuhatarisha amani katika jamii, akisema vitendo hivyo vinasababishwa na baadhi ya wafugaji.

DC Kyobya (kushoto) na John Chambi (mfugaji – kulia) – picha na: Kuruthum Mkata

Amefafanua kuwa migogoro hiyo imekuwa chanzo cha matukio ya kikatili, ikiwemo mapigano na vifo, akitolea mfano kifo cha aliyekuwa Afisa Ardhi kilichotokea hivi karibuni katika Halmashauri ya Mji wa Ifakara, sambamba na kulaani tabia ya baadhi ya wafugaji kuvamia maeneo ya wakulima na kuwapiga wananchi.

sauti ya DC Kyobya

Kwa upande wake, Kaimu Mkurugenzi wa Mji wa Ifakara ambaye pia ni Mkuu wa Idara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Dk. Yuda Mgeni, ameeleza kuwa wafugaji wanakabiliwa na changamoto mbalimbali katika shughuli zao.

Dkt Yuda Mgeni – picha na; Kuruthum Mkata