Pambazuko FM Radio

Mbunge Asenga aiomba Serikali msaada wa dharura wa chakula kwa Wahanga wa Mafuriko-Ifakara

8 April 2024, 4:42 pm

Huu sio Mto bali na Mafuriko baada ya mto Kilombero kujaa {Picha na Elias Maganga}

Mpaka sasa Mh Naibu spika zaidi ya wananchi 300 wamehifadhiwa katika baadhi ya Shule,Je serikali na Wizara inamsaidiaje kupata chakula cha dharula kwa wananchi wa Jimbo la Kilombero?“-Mbunge wa Jimbo la Kilombero Mh,Abubakar Asenga

Na Elias Maganga

Mbunge wa Jimbo la Kilombero Abubakar Asenga ameiomba serikali kutoa chakula cha dharula kwa wananchi waliokumbwa na mafuriko katika Jimbo la Kilombero hususan katika Halmashauri ya Mji wa Ifakara.

Mbunge Asenga ameliambia Bunge Jijini Dododma wakati akiuliza swali kwa Wizara ya Muungano na Mazingira kuwa mpaka sasa Zaidi ya wananchi 300 wamehifadhiwa katika baadhi ya Shule,Je serikali na Wizara inamsaidiaje kupata chakula cha dharula kwa wananchi wa Jimbo la Kilombero?

Picha ya Mbunge wa Jimbo la Kilombero Abubakar Asenga akiwa Bungeni{Picha kutoka Maktaba}
Sauti ya Mbunge Asenga

Akijibu swali hilo Bungeni Jijini Dododma Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mhe Dkt. Selemani Jafo amekiri kuwepo kwa athari nyingi zilizosababishwa na Mafuriko katika baadhi ya maeneo ikiwemo Halmashauri ya Mji wa Ifakara

Waziri Jaffo amesema kwasababu jambo hili ni la kiutu zaidi, amewaomba wadau mbalimbali hasa wa kimaendeleo kuwafikia wahanga ili kuwapatia  msaada

Picha ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mhe Dkt. Selemani Jafo{Picha kutoka Maktaba ya Bunge
Sauti ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mhe Dkt. Selemani Jafo