Pambazuko FM Radio

Wakazi wa Mlimba wapokea huduma za kibingwa za afya kwa furaha

15 October 2023, 10:11 am

Baadhi ya wagonjwa wakisubiri huduma za kibingwa -Picha na Isidory Matandula

Madaktari bingwa wa mfumo wa mkojo na  ENT (Ear, Norse and Throat) kutoka hospitali ya rufaa ya Mtakatifu Fransisko, Ifakara, wiki hii wametoa huduma za kibingwa katika Kituo cha Afya Mlimba, Halmashauri ya Mlimba, wilaya ya Kilombero, Mkoani Morogoro.

Na Isidory Matandula

Wakazi wa Mlimba halmashauri ya Mlimba wamenufaika na huduma za kibingwa kotuku kwa  madaktari bingwa wa Hospitali ya rufaa ya Mtakatifu Fransisko ya mjini Ifakara.

Mzee Bernard Mapunda na Blandina Cletus ni miongoni mwa wananchi walionufaika na hudumahiyo, ambapo  mzee mapunda amezibuliwa masikio na mtoto  Ronclif mwenye umri wa wiki mbili ameongezewa njia ya mkojo.

Mzee Mapunda – Picha na Isidory Matandula

Nta za masikioni kutoka kwa mzee Mapunda – Picha – Isidory Matandula

Sauti za wananchi waliopata huduma za afya za kibingwa

Nao madaktari bingwa Elias Marandu na Anthoni Magoda, wamesema mwitikio umekuwa mzuri, ambapo  wagonjwa walioonwa nao wamefurahi na wamenufaika   na kliniki hiyo Mkoba na wameahidi kuwa  itakuwa endelevu.

Dr. Marandu na mzee Mapunda – Picha na Isidory Matandula

sauti za madaktari bingwa – Magoda na Marandu

Kwa upande wake mganga mfawidhi wa kituo hicho, Herman Mnema Mganga, ameomba huduma hiyo ifanyike walau  mara moja kwa mwezi au kila baada ya miezi mitatu.

Mganga mfawidhi kituo cha afya Mlimba – Picha na Isidory Matandula

Sauti ya mganga Mfawidhi