Pambazuko FM Radio

Mafuriko yaua mtu mmoja Ifakara

25 March 2024, 5:31 pm

Wananchi wa Halmashauri ya Mji wa Ifakara wametakiwa kuwa makini katika kipindi hiki cha mafuriko na pia wazazi wanapaswa kuwaangalia watoto wao wasiwaache kwenda kuchezea maji kwani wanaweza kupoteza maisha

Na Elias Maganga

Baadhi ya maeneo katika Halmashauri ya Mji wa Ifakara yamekumbwa na mafuriko yaliyosababisha kifo cha kijana Shafii Abas Kambeyu mwenye umri wa miaka 19 ambaye ni dereva  Bodaboda.

Kamanda wa zimamoto na uokoaji Inspector Haji Madulika amesema Kijana huyo amefariki wakati akiwa katika shughuli zake za kusafirisha abiria asubhui ya march 25 mwaka huu.

Inspector Madulika amesema chanzo cha kifo chake  ni bodaboda kudondosha yebo  alizokuwa amevaa,baada ya kusimama ili azifuate yebo zake ndipo aliposombwa na maji ambapo mpaka sasa mwili wa kijana huyo bado haujapatikana  huku juhudi za kuutafuta zikiendelea.

Zaidi ya nyumba mia moja katika kata za Viwanja sitini,Mbasa na Katindiuka zimezingirwa na maji na serikali ikiendelea na juhudi za kuwahamisha watu kwenye nyumba zilizozingirwa na mafuriko.

Picha ya Kamanda wa zimamoto na uokoaji Wilaya ya Kilombero Inspector Haji Madulika
Sauti ya Kamanda wa zimamoto na uokoaji Wilaya ya Kilombero Inspector Haji Madulika

Diwani wa kata ya Viwanja sitini Ericky Kulita amesema taarifa za kutokea kwa mafuriko hayo alizipata saa tisa usiku,walianza kuwahamasisha wananchi kwa kushirikiana na wenyeviti kuwaondosha wananchi waliokuwa kwenye maeneo hatarishi jambo ambalo wamefanikiwa na ametoa rai wananchi kuwa waangalifu hususani katika kipindi hiki cha masika.

Sauti ya Diwani wa kata ya Viwanja sitini Ericky Kulita

Baadhi ya wananchi waliokumbwa na mafuriko katika maeneo ya kwa shungu katka Halmashauri ya Mji wa Ifakara Mandina Paulo na Salima Upuyu wamesema mafuriko hayo yamewaathiri kwa kiasi kikubwa vitu vingi yakiwemo magodoro,vyakula  na nyumba zao kuzingirwa na maji.

Picha ya Mandina Paulo na Salima wahanga wa mafuriko

Juhudi za ukoaji zinaendela kufanyika kwa ushirikiano wa jeshi la zimamoto na uokoaji ,Jeshi la polisi,Mamlaka ya usimamizi wa wanyamapori Tanzania {TAWA},Scout na Shirika la Msalaba Mwekundu Tanzania Wilaya ya Kilombero.