Pambazuko FM Radio

Dkt. Biteko aipongeza Tanesco kurejesha umeme

2 April 2024, 3:43 pm

Picha ya Naibu Waziri Mkuu Dotto Biteko akiwa katika ofisi za Tanesco Kidatu baada ya kutokea kwa hitilafu ya umeme Picha na Elias Maganga}

“Hakuna mgao  wala upungufu wa umeme kwa sasa hiki kilichotokea ni hitilafu kwenye mitambo ya kuzalisha umeme” Naibu Waziri Mkuu Dotto Biteko

Na Elias Maganga

Naibu Waziri Mkuu ambaye pia ni Waziri wa Nishati Dkt. Dotto Biteko  amelipongeza shirika la umeme Tanzania {Tanesco} kwa juhudi walizozifanya kuhakikisha umeme unarejea kutokana na hitilafu ya mitambo iliyojitokeza kuanzia majira ya saa nane usiku wa marchi 31 kuamkia april mosi mwaka huu.

Dkt Biteko ametoa pongezi hizo baada ya kufanya ziara ya dharula katika Bwawa la kufua umeme Kidatu April mosi mwaka huu ili kujionea kile kilichosababisha umeme kukatika ambapo amesema hitilafu hiyo imetokana  na mvua zilizonyesha marchi 31 mwaka huu na kupelekea mikoa kadhaa kuathirika kwa kukosekana kwa nishati hiyo.

Aidha Dkt Biteko amewatoa hofu wananchi baada ya kurejea kwa huduma ya umeme na kusema kuwa  hakuna mgao  wala upungufu wa umeme kwa sasa .

Picha ya Naibu Waziri Dotto Biteko {Picha na Elias Maganga}
Sauti ya Waziri wa Nishati Dkt Dotto Biteko

Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya kilombero wakili Dunstan Kyobya  ambaye amemuwakilisha mkuu wa Mkoa wa Morogoro Adam Malima  amewataka  watu wanaoishi mabondeni   kuhama mara moja,huku akielezea baadhi ya maeneo yaliyoathirika na maji ndani ya mkoa wa morogoro

Sauti ya Mkuu wa Wilaya ya Kilombero Wakili Dunstan Kyobya