Pambazuko FM Radio

Ushirikishwaji unahitajika zaidi utunzaji mazingira Ifakara

8 May 2026, 12:33

Picha ya Kitalu cha Miti iliyooteshwa na TFS Kilombero(Picha na Katalina Liombechi)

Wananchi wa Ifakara wameeleza kuwa licha ya kampeni za serikali na asasi mbalimbali kuhamasisha utunzaji mazingira kupitia upandaji miti, bado mwitikio wa baadhi ya jamii ni mdogo wakitaka kuongeza elimu na ushirikishwaji wa wananchi ili kuunga mkono jitihada za mazingira

Na Amina Mrisho

Licha ya serikali na asasi mbalimbali kuanzisha kampeni ya utunzaji mazingira kwa kupanda miti inaelezwa kuwa bado kumekuwa na mwitikio mdogo kwa baadhi ya wanajamii kuunga mkono jitihada hizo.

Agnes Kapama mkazi wa Mbasa kati na Nuhu Kisweka mkazi wa viwanja sitini katika Halmashauri ya mji wa Ifakara wametoa mtazamo wao kuhusu mwitikio wa wananchi juu ya upandaji wa miti.

Sauti za wananchi katika Halamashauri ya Mji wa Ifakara

Afisa mazingira Halmashauri ya mji wa Ifakara bi. Salome Mayenga akizungumza na Pambazuko FM amesema kwa sasa mwitikio wa wananchi kwenye upandaji wa miti upo juu na hii ni kutokana na hamasa na ushirikishwaji katika kukabiliana na mabadiliko ya Tabianchi.

Picha ya Salome Mayenga Afisa Mazingira Halmashauri ya Mji wa Ifakara(Picha na Katalina Liombechi)
Sauti ya Salome Mayenga Afisa Mazingira

Bi. Salome pia ameeleza mbinu mbalimbali wanazozitumia kuwahamasisha wananchi kupanda miti.

Sauti ya Salome Mayenga 2

Mdau wa Mazingira kutoka shirika AMECEA bi. Sara Pelaji ametoa wito kwa jamii kuwafundisha watoto kuwa na mahusiano na mazingira.

Sauti ya Mdau wa Mazingira