Pambazuko FM Radio
Pambazuko FM Radio
6 June 2025, 14:57

Chadema tumesema yafanyike marekebisho ya sheria ndio tuingie kwenye uchaguzi 2025
Na Elias Maganga
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA)kinaendelea na ziara yake Nchi nzima ya kuhamasisha Agenda ya kutoshiriki uchaguzi mkuu kama hakutakuwa na marekebisho makubwa ya mifumo na sheria za uchaguzi.
Akizungumza kwa nyakati tofauti wakati akiwahutubia wananchi June 5,2025 wa Halmashauri ya Mlimba kata ya Igima,ulanga kata ya Minepa na Halmashauri ya Mji wa Ifakara Kata ya Ifakara Makamu mwenyekiti wa Chama hicho John Heche amesema wanachokitaka wao kufanyike marekebisho ya sheria ili washiriki uchaguzi mkuu wa2025.

Kwa upande wake Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chedema Taifa Bi Rose Maimba amelaani utekaji na ameiomba jamii kushirikiana kulikemea .