Pambazuko FM Radio
Pambazuko FM Radio
14 August 2026, 14:41

Kuelekea wiki ya nenda kwa usalama, Jeshi la Polisi kikosi cha usalama barabarani wilaya ya Kilombero limefanya ukaguzi wa magari ya Hospitali ya rufaa ya mkoa ya Mtakatifu Fransisko pamoja na magari ya watumishi, kwa lengo la kubaini kasoro na kuimarisha usalama wa wagonjwa, watumishi na watumiaji wengine wa barabara.
Na: Isidory Mtunda
Kuelekea wiki ya nenda kwa usalama, DTO wilaya ya Kilombero, ASP Blandina Kasongwa ameendesha zoezi la ukaguzi wa magari ya Hospitali ya rufaa ya mkoa ya Mtakatifu Fransisko na watumishi, kwa mwaliko wa mkurugenzi wa Hospitali hiyo ndugu Solanus Fusi.

Akizungumza na Pambazuko radio, ASP Kasongwa amesema zoezi hilo wanaangalia mifumo yote saba ya gari ili kuona iwapo haina kasoro na ameweka bayana kuwa mmiliki wa gari anawajibika kulipia STICER ya Nenda kwa usalama kulingana na aina ya chombo.
Naye afisa utawala wa Hospitali hiyo bwana Ezekiel Joachim kwa niaba ya mkurugenzi, ameipongeza timu ya usalama barabarani wilaya ya Kilombero kwa kuendesha zoezi hilo kituoni hapo, kwani kwa kufanya hivyo kunaokoa muda wa madaktari na wauguzi kusitisha huduma kwa wagonjwa kwenda kushughulikia ukaguzi wa magari.
Kwa niaba ya wafanyakazi wa hospitali hiyo, Dkt Godfrey Ligomba ameishukuru timu ya DTO kuwafuata eneo lao la kazi, kitendo hicho kimewakolea muda na amemshukuru mkurugenzi wake kwa kuratibu zoezi hilo.