Pambazuko FM Radio
Pambazuko FM Radio
26 September 2026, 13:05
Kakakuona ana mchango mkubwa katika mfumo wa ikolojia, hasa kwa kula mchwa na wadudu wengine wadogo, hivyo kusaidia kudhibiti wadudu na kuuweka mazingira katika hali nzuri-Nick Jackson Mwanri-Afisa Wanyamapori

Kakakuona picha kwa Hisani ya Mtandao
Na Henry Mwakifuna
Mnyama aina ya kakakuona (pangolin) ameendelea kukabiliwa na uwindaji haramu barani Afrika, kutokana na imani potofu zinazomhusisha na matumizi mbalimbali ya kitamaduni ambayo hayajathibitishwa kisayansi.
Wataalamu wa uhifadhi wanasema kakakuona ana mchango mkubwa katika mfumo wa ikolojia, hasa kwa kula mchwa na wadudu wengine wadogo, hivyo kusaidia kudhibiti wadudu na kuuweka mazingira katika hali nzuri.

Akizungumza katika Kona ya Jamii ya Jioni leo inayodhaminiwa na Taasisi ya Six Rivers Africa, afisa kutoka Idara ya Wanyamapori Wilaya ya Morogoro Nick Jackson Mwanri amesema elimu zaidi inahitajika kwa jamii ili kuondoa imani potofu na kuhakikisha mnyama huyo anaendelea kuwepo kwa manufaa ya kizazi cha sasa na kijacho.
Mbali na umuhimu wake katika mazingira, kakakuona ni miongoni mwa wanyama wanaovutia watalii, huku thamani yake ikitajwa kufikia takribani dola 390 za Marekani, sawa na zaidi ya shilingi milioni moja za Tanzania.
Sikiliza kona ya Jamii Uhifadhi