Pambazuko FM Radio

Mwigulu aiagiza TAKUKURU migogoro wakulima,wafugaji

26 November 2026, 19:03

Picha ya Wakazi wa Ifakara waliojitokeza kwenye Mkutano wa Waziri Mkuu(Picha kwa hisani ya Halmashauri ya Ifakara)

Natambua ardhi haiongezeki lakini haipaswi watu kujichukulia sheria mkononi kisa mgogoro wa wakulima na wafugaji,watu wasipate kiburi kwa kuwa na uwezo wa kutoa rushwa

Na Katalina Liombechi

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba, amesema Serikali haitavumilia uvunjaji wa sheria unaofanywa kwa makusudi kutokana na migogoro kati ya wakulima na wafugaji, inayochochea visasi na vitendo vya kuwindana.

Amesema hali hiyo haikubaliki na inaweza kusababisha vifo vya makusudi, hivyo amewataka wakulima na wafugaji kuacha kujichukulia sheria mkononi na badala yake kutumia njia halali kutatua migogoro yao.

Kufuatia hayo Mh. Waziri Mkuu ameiagiza taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa TAKUKURU kuchunguza mazingira ya rushwa katika migogoro ya namna hiyo.

Picha ya Waziri Mkuu Dkt.Mwigulu Nchemba(Picha kwa hisani ya Halmashauri ya Mji wa Ifakara)
Sauti ya Waziri Mkuu

Waziri Mkuu ameyasema hayo Novemba 25, 2026, alipokuwa akizungumza na wakazi wa Ifakara, Wilaya ya Kilombero, ikiwa ni sehemu ya ziara yake mkoani Morogoro.