Pambazuko FM Radio

Vijana 27 wafundishwa fursa za uzalishaji Kokoa

5 October 2026, 10:05

Lengo ni kuwawezesha vijana kuona kilimo kama fursa ya kibiashara na njia ya kujiajiri, kuongeza kipato na kujenga uchumi wao kupitia zao la kakao–Mwenyekiti jukwa la Vijana

Baadhi ya Vijana waliopatiwa mafunzon ya uzalishaji wa Miche ya Kokoa Itomhowa Mlimba picha na Jukwaa

Na Henry Mwakifuna

Jukwaa la Vijana la Halmashauri ya Mlimba, wilayani Kilombero, limefanikisha kutoa elimu ya ujasiriamali kwa vijana 27 kutoka katika vikundi mbalimbali vya ujasiriamali vya Itongowa, Kata ya Mngeta.

Elimu hiyo imelenga kuwajengea vijana uelewa kuhusu fursa za kiuchumi zinazotokana na zao la kakao, ambalo limetajwa kuwa miongoni mwa mazao yenye uwezo wa kuchochea ajira, kuongeza kipato na kukuza uchumi wa vijana.

Vijana hao wamepatiwa elimu kuhusu fursa za zao hilo, pamoja na misingi ya kuanzisha uzalishaji wa miche ya kakao.

Aidha, vijana wameshiriki kwa vitendo katika maandalizi ya awali ya uzalishaji, hatua inayolenga kubadilisha maarifa waliyoyapata kuwa vitendo na hatimaye vitendo hivyo kuwa fursa za kiuchumi.

Hata hivyo, Mwenyekiti wa Jukwaa hilo  Gaspar Matanda amesema changamoto kubwa iliyopo ni namna ya kufikia vikundi mbalimbali vya vijana, kutokana na hali ya kiuchumi pamoja na changamoto za kijiografia zinazozikabili baadhi ya maeneo ndani ya Halmashauri ya Mlimba.

Sauti ya Mwenyekiti wa Jukwaa la Vijana Halmashauri ya Mlimba