Pambazuko FM Radio

DC Kyobya apiga Vita Mmomonyoko wa Maadili Kilombero

18 November 2026, 11:29

Baadhi ya Wajumbe walioudhuria Kiao cha Baraza la Ushauri la Wilaya DCC hivi karibuni Picha na Kuruthum Mkata

Suala la Maadili lisifumbiwe Macho katika maeneo yetu iwekwe mikakati kuhakikisha mmomonyoko wa maadili unadhibitiwa-DC Kilombero

Na Kuruthum Mkata

Mkuu wa Wilaya ya Kilombero, Wakili Dunstan Kyobya, amewataka viongozi na wananchi kutofumbia macho masuala ya mmomonyoko wa maadili katika jamii, akisisitiza umuhimu wa kuendelea kutoa elimu na kuchukua hatua za kukabiliana na vitendo vinavyokiuka maadili.

Akizungumza katika kikao cha Baraza la Ushauri la Wilaya (DCC),Dc Kyobya amesema ni muhimu kuboresha utaratibu wa utoaji wa vibali vya sherehe, kwa kuweka masharti yatakayozuia watoto kushiriki katika matukio yasiyozingatia maadili.

Wakili Dunstan Kyobya Mkuu wa Wilaya ya Kilombero akizungumza katika Kikao cha Baraza la Ushauri la Wilaya hivi karibuni Picha na Kuruthum Mkata

Sauti ya DC Kyobya

Kwa upande wake, Mkuu wa Polisi Wilaya ya Kilombero, ASP Diventine Nyahoro, amesema kuna umuhimu wa kusimamia maudhui na aina ya miziki inayopigwa katika sherehe, akiahidi kuchukua hatua dhidi ya muziki unaokiuka sheria.

Mkuu wa Polisi Wilaya ya Kilombero, ASP Diventine Nyahoro, Akizungunza Kwenye kikao cha Baraza hilo Picha na Kuruthum Mkata

sauti ya OCD Nyahoro

Naye Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mlimba, Martha Mkula, amesema halmashauri yake imeanza kudhibiti baadhi ya shughuli za muziki katika sherehe, huku akiwakemea watu wanaocheza kwa namna isiyofaa mbele ya watoto na kuwataka viongozi kushirikiana kutatua changamoto za maadili.

sauti ya Martha Mkula

Wakichangia hoja hiyo, baadhi ya viongozi wa vyama vya siasa na dini wilayani Kilombero, akiwemo Magreth Lipindi, wameunga mkono jitihada za kudhibiti sherehe za majumbani, wakishauri sherehe hizo kufanyika kwenye kumbi maalumu ili kuweka mazingira bora ya usimamizi na kuwalinda watoto dhidi ya vitendo vinavyoweza kuathiri maadili yao.