Pambazuko FM Radio
Pambazuko FM Radio
16 October 2026, 18:17

Bango la shule ya Msingi Lumemo Halmashauri ya Mji Ifakara likionesha uwapo wa Wanafunzi wenye Mahitaji Maalum Picha na Henry Mwakifuna
Bado kuna uelewa mdogo wa jamii juu ya suala la watoto wenye mahitaji maalum hivyo juhudi zaidi zinahitajika-Nasma Chande.
Na Henry Mwakifuna
Afisa Ustawi wa Jamii wa Halmashauri ya Mji wa Ifakara, Nasma Chande, amesema uelewa wa jamii kuhusu haki za watoto wenye mahitaji maalum bado ni mdogo, hali inayochangia mitazamo hasi na unyanyapaa dhidi yao.
Chande amesema kampeni mbalimbali za uhamasishaji zinaendelea kutekelezwa ili kuongeza uelewa wa jamii kuhusu haki za watoto hao na umuhimu wa kuwapatia fursa sawa katika elimu na maisha ya kila siku.
Ameutaja Mradi wa Sauti Zetu kuwa miongoni mwa juhudi zinazotekelezwa katika maeneo matano ya Mji wa Ifakara, kwa lengo la kuelimisha jamii kuhusu masuala yanayowahusu watoto wenye mahitaji maalum.
Sauti ya Afisa Ustawi
Kwa upande wao, baadhi ya wanafunzi wenye mahitaji maalum wa Shule ya Msingi Kigamboni, Halmashauri ya Mji wa Ifakara, wamesema wanakabiliwa na changamoto za unyanyapaa na upungufu wa vifaa vya kujifunzia. Wameiomba Serikali kuwasaidia ili waweze kupata elimu katika mazingira yanayowawezesha kutimiza ndoto zao.
Sauti ya Wanafunzi wenye Mahitaji Maalum
Naye mama aliyejitambulisha kwa jina la Mama Lu amesema ameshuhudia mabadiliko kwa mtoto wake, huku akiiomba Serikali kuboresha mazingira ya shule na kuhakikisha walimu wanaelewa mahitaji ya watoto wenye mahitaji maalum ili waweze kuwasaidia ipasavyo.
Sauti ya Mama mwenye mtoto mwenye Ulemavu