Pambazuko FM Radio

Wakazi Ifakara waeleza matarajio ziara ya Waziri Mkuu

23 November 2026, 19:24

Picha ya baadhi ya wakazi wa Ifakara(Picha na Katalina)

Ziara hiyo itakuwa fursa ya kufikisha changamoto zao na kupata ufafanuzi kuhusu masuala mbalimbali ya maendeleo yanayowakabili

Na Katalina Liombechi

Baadhi ya wakazi wa Halmashauri ya Mji wa Ifakara wameeleza matarajio yao kuelekea ziara ya Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba, inayotarajiwa kufanyika Novemba 25, 2026.

Wananchi hao wanatarajia ziara hiyo itakuwa fursa ya kufikisha changamoto zao na kupata ufafanuzi kuhusu masuala mbalimbali ya maendeleo yanayowakabili.

Katika ziara hiyo, Waziri Mkuu anatarajiwa kukagua miradi ya maendeleo pamoja na kuzungumza na wananchi katika viwanja vya CCM Tangani, Ifakara.

Sauti za baadhi ya wakazi wa Ifakara

Mwenyekiti wa Mtaa wa Uwanja wa Taifa B Kata ya Viwanja Sitini Adela Kalaghe ametoa wito kwa wananchi wake kujitokeza kwa wngi katika ziara hiyo akiwa Ifakara na kuzungumza na wananchi Viwanja vya CCM Tangani.

Picha ya Adela Kalaghe Mwenyekiti mtaa wa Uwanja wa taifa B (Picha na Katalina Liombechi)
Sauti ya Adela Kalaghe mwenyekiti uwanja wa taifa B

Hata hivyo utakumbuka hivi karibuni Novemba 20,2026 Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mh. Queen Sendiga akizungumza na waandishi wa Habari alielezea ziara hiyo ya siku tano mkoani Morogoro tangu Novemba 21,2026 ambapo atakagua miradi,kufanya vikao na viongozi pamoja na kuzungumza na wananchi.

Sauti ya Mkuu wa Mkoa wa Morogoro