Pambazuko FM Radio
Pambazuko FM Radio
27 October 2026, 11:13

Sehemu ya Zawadi zitakazotolewa kwa Shile washindi wa Uhifadhi Ifakara Picha na Hospice Lipipa
Tunahusisha michezo ya mpira wa miguu na mpira wa pete, kwa lengo la kuongeza uelewa wa uhifadhi wa mazingira miongoni mwa watoto na vijana kwa ajili ya kizazi kijacho-Irene Masonda.
Na Henry Mwakifuna
Shirika la Six Rivers Africa limewekeza karibu shilingi milioni tisa kwa ajili ya michezo ya wanafunzi, ikiwa ni sehemu ya kuendeleza elimu ya uhifadhi wa mazingira kwa vizazi vijavyo.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa Ligi ya Uhifadhi Mwakilishi wa Six Rivers Africa Irene Masonda amesema kuwa katika Halmashauri ya Mji wa Ifakara, shule 16 za msingi zinashiriki katika mashindano hayo.

Mratibu wa Michuano ya Uhifadhi wa Six Rivers Africa Irene Masonda akizungumza na Wanafunzi waliohudhuria Uzinduzi huo Picha na Hospice Lipipa
Amesema ligi hiyo itahusisha michezo ya mpira wa miguu na mpira wa pete, kwa lengo la kuongeza uelewa wa uhifadhi wa mazingira miongoni mwa watoto na vijana.
Katika mpira wa miguu, mshindi wa kwanza atazawadiwa shilingi milioni nne, mshindi wa pili milioni mbili na mshindi wa tatu milioni moja.
Kwa upande wa mpira wa pete, bingwa atapata shilingi milioni moja, huku mshindi wa pili akizawadiwa shilingi laki tano.
Fainali za ligi hiyo zinatarajiwa kufanyika Novemba 4, 2026.
sauti ya Mwakilishi wa Six Rivers Africa