Pambazuko FM Radio
Pambazuko FM Radio
5 November 2026, 11:35

Baadhi ya Wanafunzi waliohudhuria kwenye Michuano ya Ligi ya Uhifadhi Picha na Kuruthum Mkata
shule 16 zimeshiriki katika ligi hii na tutaendelea kushirikiana na Mamlaka na Serikali katika Kuelimisha janii juu ya Uhifadhi -Mwakilishi Six Rivers Africa.
Na Kuruthum Mkata
Shirika la Sixrivers Africa limeendelea kuhamasisha uhifadhi wa mazingira kupitia michezo kwa wanafunzi, kupitia mashindano ya Conservation Cup iliyofanyika katika viwanja vya shule ya msingi Mkasu, Kata ya Kiberere, Ifakara.
Akizungumza katika mashindano hayo Meneja matokeo kutoka sixrivers Africa Mery Malandu amesema lengo la michezo hiyo ni kutoa elimu kwa jamii kuhusu umuhimu wa kutunza hifadhi, wanyamapori na mazingira kupitia michezo.

Meneja matokeo kutoka sixrivers Africa Mery Malandu akizungumza kwenye fainali za Kombe la Uhifadhi picha na Kuruthum Mkata
Ambapo Amesema shule 16 za msingi katika Halmashauri ya Mji wa Ifakara zimenufaika na mpango huo, huku wanafunzi wakitarajiwa kufikisha elimu ya uhifadhi katika familia na jamii zinazowazunguka.
sauti ya Mwakilishi wa Six Rivers Africa

Afisa Michezo wa Halmashauri ya Mji wa Ifakara Bwana Rashid Mgaruka akizungumza wakati wakufunga Ligi ya Uhifadhi picha na Kuruthum Mkata
Kwa upande wake, Afisa Michezo wa Halmashauri ya Mji wa Ifakara Bwana Rashid Mgaruka,ambaye ndiye mgeni rasmi katika fainali hizo amepongeza mpango huo na kuahidi ushirikiano kutoka kwa Halmashauri ya mji wa ifakara , huku akiwataka wananchi kuepuka vitendo vinavyoharibu mazingira na kutoa taarifa za uharibifu.
sauti ya Afisa Michezo

Mkuu wa Kitengo cha Mahusiano TANAPA, Ahmed Nassoro kwenye Fainali ya Ligi ya Uhifadhi picha na Kuruthum Mkata
Naye Afisa Uhifadhi Mwandamizi na Mkuu wa Kitengo cha Mahusiano TANAPA, Ahmed Nassoro, amelishukuru Shirika la Sixrivers Africa kwa kuwekeza katika elimu ya uhifadhi kupitia michezo, akiahidi kuendelea kushirikiana na wadau hao.
sauti ya Mkuu wa Kitengo TANAPA
Mashindano hayo yanaongozwa na kaulimbiu isemayo “Cheza, Linda, Hifadhi.”