Pambazuko FM Radio
Pambazuko FM Radio
20 October 2026, 11:21

Picha ya Msitu picha kwa Msaada wa Mtandao
Ukiukaji huu unahusisha uvunaji, uuzaji na usafirishaji usiozingatia sheria–Mhifadhi Ntibansubile
Na Henry Mwakifuna
Katika kipindi cha Mwaka mmoja uliopita Watu 93 wamekamatwa kwa tuhuma za kujihusisha na uvunaji, usafirishaji, biashara na matumizi yasiyo halali ya mazao ya misitu.
Miongoni mwa mazao yaliyokamatwa ni mbao 1,339, slipes 600, mkaa wenye uzito wa kilogramu 9,300 pamoja na magogo 110.
Akizungumza Katika Kona ya Jamii ya Pambazuko FM, Askari Mhifadhi wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania, TFS, Frank Ntibansubile, ameeleza hatua zinazochukuliwa kudhibiti vitendo vinavyokiuka sheria na taratibu za usimamizi wa mazao ya misitu.
Kwa upande wake, Kaimu Kamanda wa Usalama Barabarani Wilaya, Staff Sajenti Godfrey Mapunda, amesema sheria inataka wasafirishaji wa mazao ya misitu kuwa na vibali vinavyohitajika na kupita katika vizuizi vilivyowekwa kisheria.
Aidha, nyaraka zinazopaswa kuzingatiwa ni pamoja na leseni ya uvunaji, risiti za malipo na ushuru wa mazao ya misitu, kulingana na taratibu husika.
Wito umetolewa kwa wote wanaojihusisha na uvunaji na usafirishaji wa mazao ya misitu kuzingatia sheria na taratibu zilizowekwa ili kusaidia kulinda rasilimali za misitu nchini.
Nao baadhi ya Watumiaji wa Pikipiki maarufu kama Boda Boda wamekiri kusafirisha mazo ya Misitu bila kujua Taratibu na baadhi wameshawahi kukamatwa
sikiliza sehemu ya Kona ya Jamii