Pambazuko FM Radio
Pambazuko FM Radio
10 October 2026, 08:52
jukumu la kulinda mazingira ni la kila mtu, hususan jamii zinazoishi karibu na maeneo ya hifadhi-Isabella Kyamba.

Bi Isabella Kyamba, kutoka Taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori Tanzania (TAWIRI) Iringa, Kitengo cha Maabara ya Wanyamapori, akizungumza kupitia Pambazuko FM Picha na Henry Mwakifuna
Na Henry Mwakifuna
Isabella Kyamba, kutoka Taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori Tanzania (TAWIRI) Iringa, Kitengo cha Maabara ya Wanyamapori, amesisitiza umuhimu wa uchunguzi wa kisayansi katika kulinda afya ya jamii na kuimarisha uhifadhi wa mfumo wa ikolojia.
Ameieleza Jamii kupitia Pambazuko FM Katika Ukifadhi kuwa ni muhimu kufuatilia mabadiliko yoyote yanayotokea katika mazingira na kutoa taarifa kwa wakati ili kuwezesha hatua za haraka za uhifadhi. Amesisitiza kuwa jukumu la kulinda mazingira ni la kila mtu, hususan jamii zinazoishi karibu na maeneo ya hifadhi.

Bi Isabella Kyamba, kutoka Taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori Tanzania (TAWIRI) Iringa, Kitengo cha Maabara ya Wanyamapori, akisisitiza Jambo alipoongea na Pambazuko FM Picha na Henry Mwakifuna
Kyamba amehimiza wananchi kushiriki katika ulinzi wa mazingira kwa kuzingatia njia sahihi za uhifadhi na kutoa taarifa mapema wanapoona viashiria vya mabadiliko yanayoweza kuhatarisha wanyamapori, mazingira na afya ya jamii.
Sauti ya Isabella kyamba