Pambazuko FM Radio
Pambazuko FM Radio
2 September 2026, 14:02

“Tunaishukuru Serikali kutufikishia umeme katika kitongoji chetu itatusaidia kukuza biashara, viwanda vidogo na shughuli za ujasiriamali.”-Wananchi Ikwambi
Na Kuruthum Mkata.
Wananchi wa Kitongoji cha Ikwambi, Kijiji cha Sululu, Kata ya Signal wilayani Kilombero, wameishukuru Serikali kwa kuwafikishia huduma ya umeme wakisema itasaidia kukuza biashara, viwanda vidogo na shughuli za ujasiriamali.

Akizindua huduma hiyo, Mkuu wa Wilaya ya Kilombero Wakili Dunstan Kyobya amewataka wananchi kutumia fursa ya umeme kuanzisha miradi ya uzalishaji na viwanda vidogo vitakavyoongeza ajira kwa vijana na kukuza uchumi wa eneo hilo.

Kwa upande wake, Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Ifakara, Bw. Said Majaliwa, amehimiza wananchi kutumia umeme kwa shughuli za uzalishaji na kuchangamkia mikopo ya halmashauri ili kuendeleza miradi ya maendeleo.
Naye Kaimu Meneja wa TANESCO Mkoa wa Morogoro Kusini Eng Hassani Sesala amewataka wananchi kutunza miundombinu ya umeme na kuitumia huduma hiyo kujiongezea kipato kupitia shughuli mbalimbali za kiuchumi.
