Pambazuko FM Radio

DC Kilombero aagiza wanaoishi mabondeni kuhama

8 September 2026, 13:15

Kamati ya usalama katika kikao cha El Niño – picha na: Kuruthum Mkata

DC Kilombero awataka wananchi wanaoishi mabondeni kuhama mapema na kujiandaa kukabiliana na athari za mvua za El Niño.

Na: Kuruthum Mkata

Mkuu wa Wilaya ya Kilombero, Wakili Dunstan Kyobya, amewataka Watendaji wa Kata, Vijiji na Vitongoji kubainisha kaya zote zinazoishi katika maeneo ya mabondeni na kuzihamasisha kuhama mapema kuelekea maeneo salama, kutokana na uwezekano wa mvua za El Niño.

Amesema viongozi hao wanapaswa kushirikiana na Kamati za Maafa kutoa elimu kwa wananchi kuhusu tahadhari zinazopaswa kuchukuliwa ili kupunguza athari zinazoweza kusababishwa na mvua hizo.

mkuu wa wilaya ya Kilombero – wakili Dunstan Kyobya – picha na Kuruthum Mkata

Aidha, amezitaka Halmashauri za Mlimba na Ifakara kubaini maeneo salama yatakayotumika kuwaweka wananchi endapo maafa yatatokea, huku akisisitiza umuhimu wa kusafisha na kuzibua mitaro ili kupunguza hatari ya mafuriko.

sauti ya mkuu wa wilaya ya Kilombero wakili Dunstan Kyobya

Kwa upande wake, Meneja wa TMA Kituo cha Mahenge, Denis Ngowi, amesema wananchi wanapaswa kuanza maandalizi mapema ili kupunguza madhara yanayoweza kusababishwa na mvua za El Niño.

Meneja TMA kituo cha Mahenge – Denis Ngowi – picha na: Kuruthum Mkata

Amesema mvua hizo zinatarajiwa kuanza mwezi Oktoba katika Wilaya ya Kilombero na maeneo mengine, hivyo wananchi wanapaswa kufuata ushauri unaotolewa na wataalamu wa hali ya hewa.

sauti ya Denisi Ngowi