Pambazuko FM Radio
Pambazuko FM Radio
23 April 2026, 13:59

Afisa Mtendaji Kata ya Idete Halmashauri ya Mlimba Bi Esther Nyasebwa akiongoza zoezi la ugawaji wa vyandarua
Vyandarua hivi mnavyopewa na serikali lengo lake ni kuboresha afya zenu ili kujikinga na Malaria-Bi.Esther Nyasebwa,Mtendaji wa Kata
Na Kuruthum Mkata
Mtendaji Kata ya Idete, Halmashauri ya Mlimba Wilayani Kilombero mkoani Morogoro, ameongoza zoezi la ugawaji wa vyandarua kwa wananchi wa kata hiyo
Akizungumza wakati wa zoezi hilo, Mtendaji wa Kata hiyo Bi.Esther Nyasebwa, amesema kuwa zaidi ya kaya 200 zimefanikiwa kupatiwa vyandarua kwa lengo la kuboresha afya zao.
Aidha ameishukuru serikali kwa kuendelea kuwajali wananchi kwa kuwapatia huduma muhimu za afya, ikiwemo usambazaji wa vyandarua.

Baadhi ya Wanafunzi wa shule ya sekondari ya Matundu Hill wakigaiwa vyandarua(Picha na Kuruthum Mkata)